Featured Kitaifa

KIKAO CHA SEKRETARIETI YA SJMT NA SMZ KINACHOSHUGHULIKIA MASUALA YA MUUNGANO CHAFANYIKA ZANZIBAR

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Bw. Thabit Idarous Faina akiongoza Kikao cha Sekretarieti ya Kamati ya Pamoja cha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ya kushughulikia masuala ya Muungano kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Vuga, Zanzibar leo tarehe 17/02/2022. Kushoto ni Mwenyekiti Mwenza wa Kikao hicho Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Ngelela Maganga. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Muungano Bw. Sigsbert R. Kavishe na Bi. Siajabu Pandu Mkurugenzi wa Uratibu wa Shughuli za Serikali katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.

Picha ikionyesha wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia mjadala katika Kikao cha Sekretarieti ya Kamati ya Pamoja ya SJMT na SMZ ya kushughulikia masuala ya Muungano kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Vuga, Zanzibar

Sehemu ya wajumbe kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifuatilia mjadala katika Kikao cha Sekretarieti ya Kamati ya Pamoja SJMT na SMZ ya kushughulikia masuala ya Muungano kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Vuga, Zanzibar leo tarehe 17/02/2022. Kulia ni Bw. Mussa H. Ali, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu na Bw. Seif Sh. Mwinyi Katibu Mkuu Wizara ya Nchi, Afisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala bora.

Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Thabit Idarous Faina (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Ngelela Maganga na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) mara baada ya kukamilika kwa kikao cha Sekretariet ya Kamati ya Pamoja SJMT na SMZ ya kushughulikia masuala ya Muungano kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Vuga, Zanzibar 

About the author

mzalendoeditor