Featured Kitaifa

MASHINDANO YA RIADHA YAANZA KUTIMUA VUMBI FEASSSA 2024

Written by mzalendo

Na Angela Msimbira UGANDA

TIMU za riadha kwenye mashindano ya FEASSSA 2024 yanayofanyika Mji wa Mbale, nchini Uganda zimeanza kupamba moto huku Tanzania ikianza vyema kwa kupata medali tatu za Dhahabu, saba za Fedha na 23 za Shaba.

Agosti 23, 2024, katika mbio za mita 100 upande wa wavulana Baraka Senjigwa ameibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza akifuatiwa na mwanariadha wa Kenya ambaye ameshika nafasi ya pili na nafasi ya tatu ni wenyeji Uganda.

Kwa upande wa mbio za mita 400 msichana Grace Charles amekuwa kinara kwenye mashindano hayo akifuatiwa na Kenya aliyeshika nafasi ya pili huku wenyeji Uganda wakishika nafasi ya tatu.

Aidha, mchezo mwingine uliochezwa leo ni wa kurusha mkuki na nafasi ya kwanza imeshikwa na mchezaji wa Tanzania Pascal Qorijo na kujinyakulia medali ya dhahabu.

Michezo mingine iliyochezwa leo kwenye mashindano hayo ni mbio za kupokezana vijiti(midley relay,mbio za mita 100, 400, 3000, 1500 kurusha mkuki na miruko mitatu.

About the author

mzalendo