Featured Kitaifa

BIL. 843 ZAJENGA HOSPITALI ZA WILAYA 129 NCHINI

Written by mzalendo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kwa kipindi cha miaka 3 ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan shilingi Bili. 843 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya 129 nchini kote.

Waziri Mchengerwa ameyasema hayo mbele ya Mhe. Rais Dkt. Samia wakati akizindua hospitali ya Wilaya ya Gairo leo tarehe 02.08.2024.

Amesema Mhe. Rais tunashukuru kwa fedha nyingi ulizotoa takribani shilingi bilioni 843 kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za Afya, fedha hizo tulizipokea na zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa hospitali za Wilaya 129 na hadi kufikia sasa Wilaya zote nchini zina Hospitali za Wilaya.

Aidha Fedha hizo pia zimetumia kununua vifaa Tiba vya Shilingi Bilioni 283 na zaidi kutoka katika fedha hizo shilingi Bilioni 4.1 zimetumika kusomesha wataalam wa Afya 570.

Na hapa Gairo ni miongoni mwa Wilaya zilizonufaika na fedha hizo ulizotoa ambapo ujenzi wa majengo 16 umekamilika kwa gharama ya Shilingi Bilioni 3.5 na yanatoa huduma na zaidi fedha zingine zimetumika kwa ajili ya ununuzi wa vifaa Tiba.

Aliongeza kuwa mpaka sasa wananchi zaidi ya 12,335 wamepata huduma katika Hispitali hii wakojumuisha wananchi 700 waliopata ajali ambao wametibiwa katika jengo hili la kutolea huduma za dharura (EMD), na wakinamama 800 wameweza kujifungua katika Hospitali hii.

Rais Mhe. Dkt. Samia katika siku yake ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoani Morogoro amezindua Hospitali ya Wilaya ya Gairo.

About the author

mzalendo