Featured Kimataifa

KIONGOZI WA HAMAS AUWAWA KATIKA SHAMBULIO NCHINI IRAN

Written by mzalendo

Kundi la Hamas, limethibitisha kuuawa kwa kiongozi wake Ismail Haniya, katika shambulio linalodaiwa kutekelezwa na Israel mjini Tehran, Iran, ambako alienda kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mpya.

Katika tarifa yake, kundi hilo limesema Kaka na kiongozi wa vuguvugu lao Ismail Haniya, ameuawa katika shambulio la Kizayuni lililolenga makazi yake mjini Tehran baada ya kuhudhuria kuapishwa kwa rais mpya.

Taarifa ya Hamas pia imethibitishwa na jeshi la Iran, ambalo limethibitisha makazi ya kiongozi huyo wa juu wa Hamas kushambulia, katika tukio ambalo wanalichunguza.

Kuuawa kwake kumeibua maswali zaidi kuhusu mustakabali wa amani kwenye eneo la Gaza, hasa kwa kuwa Haniya ndiye aliyekuwa akiongoza mazungumzo ya amani.

Aidha haifahamiki ni namna gani nchi ya Iran itajibu kilichofanywa na Israel, ambayo ni wazi sasa itakuwa Katia hali ya tahadhari zaidi.

Haniya, alichukua uongozi wa kundi hilo kutoka kwa Sheikh Ahmed Yassin, ambaye aliuawa katika mashambulio ya Israel mwaka 2004. 

About the author

mzalendo