Watumishi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wakiwa katika mazoezi ya matembezi wakati wa Bonanza la Nishati ambalo limefanyika leo Julai 27,2024 Jijini Dodoma likibebwa na Kaulimbiu Shiriki Michezo Imarisha Afya.
Watumishi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wakifanya mazoezi mbalimbali wakati wa Bonanza la Nishati ambalo limefanyika leo Julai 27,2024 Jijini Dodoma likibebwa na Kaulimbiu Shiriki Michezo Imarisha Afya.
Watumishi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wakicheza michezo mbalimbali wakati wa Bonanza la Nishati ambalo limefanyika leo Julai 27,2024 Jijini Dodoma likibebwa na Kaulimbiu Shiriki Michezo Imarisha Afya.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe, Dkt. Doto Biteko,akizungumza na Watumishi wa Wizara ya
Nishati na Taasisi zilizo chini yake waliposhiriki kwenye Bonanza la Nishati ambalo limefanyika leo Julai 27,2024 Jijini Dodoma likibebwa na Kaulimbiu Shiriki Michezo Imarisha Afya.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe, Dkt. Doto Biteko,akizungumza na Watumishi wa Wizara ya
Nishati na Taasisi zilizo chini yake waliposhiriki kwenye Bonanza la Nishati ambalo limefanyika leo Julai 27,2024 Jijini Dodoma likibebwa na Kaulimbiu Shiriki Michezo Imarisha Afya.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe, Dkt. Doto Biteko,akizungumza na Watumishi wa Wizara ya
Nishati na Taasisi zilizo chini yake waliposhiriki kwenye Bonanza la Nishati ambalo limefanyika leo Julai 27,2024 Jijini Dodoma likibebwa na Kaulimbiu Shiriki Michezo Imarisha Afya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe.Jenista Mhagama,akizungumza na Watumishi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo walioshiriki katika Bonanza la Nishati ambalo limefanyika leo Julai 27,2024 Jijini Dodoma likibebwa na Kaulimbiu Shiriki Michezo Imarisha Afya.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga,akizungumza na Watumishi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo walioshiriki katika Bonanza la Nishati ambalo limefanyika leo Julai 27,2024 Jijini Dodoma likibebwa na Kaulimbiu Shiriki Michezo Imarisha Afya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba ,akizungumza na Watumishi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo walioshiriki katika Bonanza la Nishati ambalo limefanyika leo Julai 27,2024 Jijini Dodoma likibebwa na Kaulimbiu Shiriki Michezo Imarisha Afya.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Dkt. James Andilile,akizungumza mara baada ya EWURA kuibuka Mshindi wa Jumla katika bonanza hilo walioshiriki katika Bonanza la Nishati ambalo limefanyika leo Julai 27,2024 Jijini Dodoma likibebwa na Kaulimbiu Shiriki Michezo Imarisha Afya.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi.Rosemary Senyamule,akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma wakati wa Bonanza la Nishati ambalo limefanyika leo Julai 27,2024 Jijini Dodoma likibebwa na Kaulimbiu Shiriki Michezo Imarisha Afya.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe, Dkt. Doto Biteko,akikabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Dkt. James Andilile Kombe mara baada ya EWURA kuibuka Mshindi wa Jumla katika Bonanza la Nishati ambalo limefanyika leo Julai 27,2024 Jijini Dodoma likibebwa na Kaulimbiu Shiriki Michezo Imarisha Afya.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe, Dkt. Doto Biteko,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki Bonanza la Nishati ambalo limefanyika leo Julai 27,2024 Jijini Dodoma likibebwa na Kaulimbiu Shiriki Michezo Imarisha Afya.
Na.Alex Sonna-DODOMA
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk. Dotto Biteko amewaagiza watumishi wa wizara yake kutumia bonanza la michezo la wizara hiyo litakalokuwa likifanyika kila mwaka mara baada ya bunge la bajeti kuhamasishana ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Dk. Biteko alisema hayo leo Julai 27,2024 jijini Dodoma, wakati akizunguza na watumishi wa wizara hiyo wakati wa kufunga bonanza la michezo mbalimbali lililojumuisha watumishi wa wizara ya Nishati pamoja na taasisi zake.
Dkt.Biteko amesema kuwa bonanza hilo litakuwa likifanyika kila mwaka mara baada ya bunge la bajeti likiwa na lengo la watumishi kuhamasishana kutoa huduma bora kwa wananchi.
“Utaratibu huu wa bonanza utakuwa kila mwaka lengo likiwa ni kuhamasishana kutoa huduma bora kwa wananchi,” alisema Dk. Biteko.
Aidha amewataka watumishi wa wizara hiyo kupendana na kushirikiana katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ili kufikisha huduma bora kwa waananchi.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama,ameipongeza wizara hiyo kwa uratibu mzuri wa bonanza la michezo lililojumuisha taasisi zote.
“Niwapongeze sana nimefurahi kuona bonanza hili limefanikiwa sana jambo hilo sio jambo dogo kwani mmeendeleza kuitikia wito wa Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwani kiu yake ni kuona watanzania wanakuwa na afya njema.
“Kupambana na magonjwa yasiyoyakuambukiza dawa yake ni mazoezi na mazoezi huezi kuanza siku moja ni lazima uanze taratibu na tunakushukuru Naibu waziri mkuu kwa kuwa chachu na kutekeleza azma hii,” amesema Mhe. Mhagama.
Kadhalika, amesema michezo inajenga, umoja hivyo anaamini kuwa jambo hilo litawajengea maarifa mapya ya kwenda kuwatumikia watanzania katika majukumu yao ya kila siku.
Naye Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amemshukuru Dkt. Biteko kwa kuanzisha Bonanza hilo ambalo amesema linadumisha upendo miongoni mwa Watumishi, umoja, kuwawezesha wafanyakazi kufahamiana zaidi na kuwaimarisha Watumishi.
“Naamini Watumishi wamepata motisha ya kazi kupitia bonanza hilo pamoja na hamasa ya kujipanga na kujiimarisha kwa ajili ya michezo inayofuata.”amesema
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nisahati, Dk. James Andilile amesema bonanza hilo lilikuwa na mwitikio mkubwa wa watumishi wakiongozwa na wakuu wote wa taasisi za wizara ya Nishati.
“Sababu iliyotufanya tukusanyike pamoja ni kujali afya zetu kwani afya ndio mtaji wa kila kitu bila kuwa na afya njema huwezi kufanya kitu chochote,” amesema Dk. Andilile
Hata hivyo, amesema mazoezi hayo yatawapa nguvu na ufahamu wa kuongeza kasi ya kutatua changamoto zilizopo katika wizara hiyo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi.Rosemary Senyamule, naye ameipongeza Wizara ya Nishati kwa kufanya Bonanza hilo mkoani Dodoma hali ambayo imezidi kulifaharisha Jiji la Dodoma na kuchagiza uchumi
Ameahidi kuwa, Serikali mkoani Dodoma itaendelea kuwahamasisha wananchi kufanya mazoezi kama ambavyo Viongozi Wakuu wa Nchi wanahimiza ili kuimarisha afya.