Featured Kimataifa

WASANII WA TANZANIA WAKUTANA NA STAR WA KOREAN DRAMA ‘Son Ye-jin

Written by mzalendo

BALOZI wa Tanzania nchini Korea, Togolani Edriss Mavura ameambatana na wasanii aliowaalika kufanya ziara nchini Korea kusini na kukutana na msanii mkubwa nchini humo Ye-Jin kwa lengo kuimarisha mahusiano na kubadilishana ujuzi katika soko la filamu na kubadilishana mawazo ya namna ya kuendeleza sekta hiyo kimataifa.

Aidha wamekutana na na watengeneza filamu wakubwa Cheol-ha Lee na Yohwan KIM.

Director Cheol-ha Lee amesema yupo katika maandalizi ya filamu itakayohusisha waigizaji wa kimataifa’International’ na angependa kupata muigizaji kutoka Tanzania kwa Afrika.

Katika kikao hicho wasanii hao wametoa mawazo mbalimbali ikiwemo Serikali kuweka nguvu katika kuinua wasanii wadogo ili kukuza na kuendeleza vipaji.

Aidha wamepokea mwaliko kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan, kuja Tanzania kuchagua maeneo mbalimbali ya kufanyia filamu zao na kisha kutembelea vivutio maridhawa vinavyopatikana Tanzania.

Wameshukuru kwa zawadi za shuka za kimasai walizovalishwa na kiongozi wa msafara Steve nyerere, msanii Irene Uwoya na Blandina Chagula (Johari).

              

About the author

mzalendo