Na MWANDISHI WETU,
Dodoma. Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na
kufanya mazungumzo na Bw. Masha Mshomba, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), baada ya kuhitimisha Bunge Jijini
Dodoma, tarehe 28 Juni, 2024.Mazungumzo hayo yalihusu
utaratibu wa ulipaji mafao ambao NSSF imeendelea kuuboresha kupitia
mifumo ya TEHAMA.
Aidha, Bw. Mshomba ameelezea maandalizi ya ulipaji
mafao kwa kuzingatia maboresho ya kanuni ya kikokotoo, na ameipongeza
Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kujali maslahi ya
watanzania.
Pamoja na hayo, Bw. Mshomba alitumia fursa
hiyo kumpongeza Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa kuhitimisha Bunge la Bajeti
kwa mafanikio makubwa.
hiyo kumpongeza Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa kuhitimisha Bunge la Bajeti
kwa mafanikio makubwa.