Featured Kitaifa

TUCTA YAIPONGEZA SERIKALI KUHUSU KIKOKOTOO,YASHAURI MABORESHO YAFANYIKE PIA KWA SEKTA BINAFSI

Written by mzalendoeditor

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limeipongeza Serikali kwa kuongeza kiwango cha malipo ya mkupuo ya Pensheni kwa Wastaafu kutoka asilimia 33 ya sasa mpaka 40 kwa wafanyakazi waliokuwa wanapokea asilimia 50 kabla ya mifuko kuunganishwa na asilimia 35 kwa watumishi ambao walikua wakipokea asilimia 25 kabla mifuko hiyo kuunganishwa.

Pongezi hizo zimetolewa na Rais wa TUCTA, Ndg. Tumaini Peter Nyamhokya katika mkutano na Waandishi wa Habari Mjini Morogoro wakati wa Kikao cha Kamati ya Utendaji cha Shirikisho hilo ambapo alieleza kuwa, Nyongeza hizo zitapunguza kwa kiasi kikubwa malalamiko ya wafanyakazi ambayo yamekuwepo kuhusu Kikokotoo cha awali.

“ Kipekee sana tunampongeza Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kusikia kilio hiki cha muda mrefu cha watumishi, ameonesha mapenzi yake kwetu. Ni matumaini yetu kwamba baada ya mwanzo huu mzuri basi hali itakapokaa sawa asilimia hizi zitaongezeka kufikia 50.

Watumishi hawa wote ni kundi moja la wafanyakazi hii inatokana na ukweli kwamba watumishi wa UMMA waliokuwa PPF mfuko wao ulikuwa imara na baada ya kuunganishwa umesaidia kufungua mfuko wa PSSSF lakini hao wanachama ndio sasa imependekezwa walipwe mkupuo wa asilimia 35 na wenzao wanalipwa asilimia 40” Amesema Nyamhokya.

About the author

mzalendoeditor