Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza na waandishi wa Habari mkoani Kigoma leo tarehe 22 Juni, 2024 kuhusiana na kusogezwa mbele kwa uzinduzi wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambapo sasa utafanyika tarehe 20 Julai, 2024 mkoani Kigoma.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza na waandishi wa Habari mkoani Kigoma leo tarehe 22 Juni, 2024 kuhusiana na kusogezwa mbele kwa uzinduzi wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambapo sasa utafanyika tarehe 20 Julai, 2024 mkoani Kigoma.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza na waandishi wa Habari mkoani Kigoma leo tarehe 22 Juni, 2024 kuhusiana na kusogezwa mbele kwa uzinduzi wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambapo sasa utafanyika tarehe 20 Julai, 2024 mkoani Kigoma. Pamoja na e ni Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji wa Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza na waandishi wa Habari mkoani Kigoma leo tarehe 22 Juni, 2024 kuhusiana na kusogezwa mbele kwa uzinduzi wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambapo sasa utafanyika tarehe 20 Julai, 2024 mkoani Kigoma. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi. Giveness Aswile.
Baadhi ya wajumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) wakiwa katika mkutano huo leo.
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
****************
Na. Mwandishi Wetu, Kigoma.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kusogezwa mbele kwa zoezi la uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura hadi tarehe 20 Julai, 2024 badala ya tarehe 01
Julai, 2024 iliyopangwa hapo awali.
Akizungumza
na waandishi wa habari mkoani Kigoma leo tarehe 22 Julai, 2024, Mwenyekiti wa
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele amesema kwamba uzinduzi wa zoezi hilo utafanyika
siku hiyo ya Jumamosi tarehe 20 Julai, 2024 mkoani Kigoma ambapo mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim
Majaliwa Majaliwa (MB).
Mhe.
Mwambegele ameeleza kwamba uamuzi huo wa Tume umetokana na kuzingatiwa kwa
maoni ya wadau walioyatoa wakati wa mikutano iliyofanyika Jijini Dar es Salaam
na Mkoani Kigoma.
“Tume
imezingatia maoni na ushauri wa wadau. Hivyo, zoezi la uboreshaji wa Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura litaanza tarehe 20 hadi 26 Julai, 2024 badala ya tarehe
01 hadi 07 Julai, 2024, mkoani Kigoma na uzinduzi utafanyika siku hiyo ya
tarehe 20 Julai, 2024 mkoani Kigoma ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb),”
amesema.
Akizungumzia
maoni hayo ya wadau, Mhe. Mwambegele amesema Tume imefanya mikutano tisa ya
wadau ngazi ya Taifa mkoani Dar es Salaam kati ya tarehe 07 hadi 15 Juni, 2024
na mkutano mmoja wa wadau ngazi ya mkoa kwa mkoa wa Kigoma uliofanyika tarehe
19 Juni 2024.
Amewataja
wadau waliokutana na Tume kuwa ni pamoja na Viongozi wa Vyama vya Siasa,
Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya
habari, Waandishi wa habari, Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri,
Wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu, wanawake na
Wazee wa Kimila.
“Vyama vya
siasa vilitoa maoni na ushauri wa kupatiwa muda wa kutosha kwa ajili ya
kuwapata mawakala wa uandikishaji ili mawakala hao waweze kushiriki katika
zoezi kikamilifu. Aidha, vyama viliishauri Tume isogeze mbele muda wa kuanza
kwa zoezi la uboreshaji ili kutoa fursa kwa wao kuhamasisha wananchi na wafuasi
wao kujitokeza katika zoezi hilo,” amesema Jaji Mwambegele.
Amewataja
wadau wengine waliotoa maoni kuwa ni pamoja na taasisi na Asasi zilizoomba
kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uboreshaji ambazo zilieleza kuwa
kibali kinapotolewa na Tume huwa ni muda mfupi kufikia zoezi la uboreshaji
kuanza na wakashauri Tume ione namna ya kutoa kibali kwa muda utakaowawezesha
kupata fedha kutoka kwa wafadhili ili zoezi likianza nao waanze kutoa elimu
hiyo.
Kwa upande wa
Taasisi na Asasi zilizoomba kibali cha kuwa waangalizi wa uandikishaji wakati
wa uboreshaji, zilieleza kuwa kibali kinapotolewa na Tume huwa ni muda mfupi
kufikia zoezi la uboreshaji kuanza na wakashauri Tume ione namna ya kutoa
kibali kwa muda utakaowawezesha kupata fedha kutoka kwa wafadhili ili zoezi
likianza nao waanze kazi ya kutazama namna zoezi linavyoendeshwa.
Maoni mengine
ya wadau yaliyopelekea Tume kufikia uamuzi huo wa kusogeza mbele tarehe ya kuanza
na kuzindua uboreshaji wa Daftari ni yale ya kuishauri Tume ijipe muda wa
kutosha kutoa elimu ya mpiga kura kwa wadau na wananchi kabla ya kuanza kwa
zoezi lenyewe, ili wananchi wengi waweze kuelewa zoezi husika na hivyo
kuwawezesha kujitokeza kwa wingi wakati zoezi litakapoanza.