Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Nicholas Merinyo Mkapa ametembelea maabara ya Chuo Kikuu cha Hanyang kilichopo katika mji wa Seoul, Korea Kusini Juni 7, 2024
Bw. Mkapa ametembelea chuo hicho ambacho ni cha mfano katika masuala ya TEHAMA nchini Korea Kusini ambapo pamoja na teknolojia nyingine pia amekuta robot aliyetengenezwa na wanafunzi wa chuo hicho.
Katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu ameambatana na wataalam wa masuala ya TEHAMA kutoka Tanzania kwa ajili ya kujionea aina mbalimbali za teknolojia zinazotolewa katika Chuo hicho ambazo kwa kiasi kikubwa ndio zitakayotumika katika Chuo Mahiri cha TEHAMA kinachotarajiwa kujengwa jijini Dodoma.
Mapema Januari, 2024 Serikali ya Tanzania ilianza mchakato wa Ujenzi wa Chuo Mahiri hicho cha TEHAMA katika eneo la Nala jijini Dodoma.
Sambamba na hilo Naibu Katibu Mkuu huyo ametembelea pia Kituo cha kuhifadhi taarifa cha Kakao ambacho teknolojia iliyotumika itakuwa ni sehemu katika Chuo Mahiri cha TEHAMA kitakachojengwa jijini Dodoma.