Na Gideon Gregory, Dodoma.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax amesema Wizara kupitia Jeshi Ia Kujenga Taifa (JKT) imeendeIea kuwapatia vijana wa Kitanzania mafunzo ya ukakamavu, kuwajengea uzaIendo na umoja wa kitaifa, na stadi
za kazi ambapo idadi ya waIiopatiwa mafunzo imeongezeka kutoka 26,000 Mwaka wa Fedha 2022/23 hadi kufikia 52,119 Mwaka wa Fedha 2023/24.
Waziri Dkt. Tax ameyasema hayo leo Mei 20,2024 Bungeni Jijini wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2024/25 na kuongeza kuwa kati yao wavuIana ni 31,256 na wasichana ni 20,863.
“Aidha, vijana 12,000 wa kujitoIea wanaendeIea kupatiwa mafunzo katika makambi mbaIimbaIi za JKT”,amesema.
Aidha, Dkt. Tax ametoa rai kwa wananchi kutovamia maeneo ya Jeshi kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha usaIama wa maisha yao, kutokana na shughuIi za kijeshi zinazofanyika katika maeneo hayo, ikiwemo mafunzo na mazoezi mbaIimbaIi ambayo yanatumia risasi za moto, miIipuko na zana zenye mionzi.
Amesema kufanya uvamizi katika maeneo hayo, ni kuhatarisha usaIama wa Taifa, na kukwamisha shughuIi muhimu za kuIiweka tayari Jeshi kukabiIiana na matishio yoyote yanayoweza kujitokeza.
“JWTZ inamiIiki maeneo ya kimkakati katika mikoa mbaIimbaIi nchini ambayo yametengwa maaIum kwa matumizi ya kijeshi”,amesema.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax ameliomba Bunge Iiidhinishe kiasi cha Shillingi Trilioni 3. 32 katika Mwaka wa Fedha 2024/25.