Featured Kitaifa

MUHIMBILI KUJENGA HOSTELI ZA KUFIKIA NDUGU WA WAGONJWA

Written by mzalendo

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema Hospitali ya Taifa Muhimbili, tayari imeandaa mpango wa uendelezaji wa eneo la Hospitali (Master plan) ambapo mojawapo ya maeneo yatakayokuwepo kwenye mpango huo ni kujenga hosteli za bei nafuu ambazo ndugu wa wagonjwa.

Dkt. Mollel amebainisha hayo leo Jijini Dodoma wakati akijibu swali Namba374 kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Hawa Subira Mwaifunga aliyeuliza Je ni lini Serikali itatenga eneo maalum katika hospitali za Muhimbili na MOI kwa ajili ya watu wasio na ndugu Dar es salaam wanaopeleka wagonjwa kupata matibabu.

Dkt. Mollel ameeleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2024/25 Hospitali ya MOI imeandaa mpango wa mashirikiano na sekta binafsi ili ndugu wasio na mahala pa kulala toka ndani na nje ya nchi waweze kupokelewa katika hosteli zilizo karibu na Muhimbili kwa gharama nafuu.

About the author

mzalendo