Featured Kitaifa

PWANI YAINGIA MIKATABA YA UWEKEZAJI WA ARDHI KWA AJILI YA VIWANDA UKUBWA WA HEKARI 2,500

Written by mzalendoeditor

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
Wananchi wameaswa kutumia, fursa zilizopo Eneo la uwekezaji la Kwala wilayani Kibaha mkoani Pwani ,kwa ajili ya soko la kuuza malighafi mbalimbali.
Wito huo ni baada ya kuingia mikataba ya uwekezaji wa ardhi kwa ajili ya kujenga viwanda lenye ukubwa wa hekari 2,500.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara, Dkt.Ashatu Kijaji wakati wa hafla ya kukabidhi kiwanja namba 1 kitalu B kwenye eneo hilo la Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kwa mwekezaji wa kampuni ya Sino Tan (Kibaha Industrial Park Ltd) kwa ajili ya Kongani ya viwanda.
Dkt.Kijaji amesema ,Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimevunja rekodi kwa kusajili miradi 266 katika kipindi cha mwaka mmoja ikiwa ni usajili wa miradi mingi ya uwekezaji kwa kipindi kifupi cha mwaka mmoja.
Pia amebainisha kuwa,wingi wa miradi hiyo haijawahi kusajiliwa kwa muda mfupi ndani ya mwaka mmoja tangu nchi imepata Uhuru ambapo uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan umefanya hayo ndani ya mwaka mmoja .
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara, Profesa Tobias Kaiyarara amesema kuwa, upatikanaji wa ardhi ni jambo kubwa kuliko kitu chochote ndiyo maana sheria zinabadilishwa ili ardhi ipatikane haraka ili mradi ufanyike kwa haraka.
Mwakilishi wa wa Sino Tan Kibaha, Jensen Huang amesema kuwa, mradi huo umegharimu dola za Marekani milioni 150 ikiwa ni gharama za upatikanaji ardhi, miundombinu na vifaa na utatoa ajira 100,000 za moja kwa moja.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Abubakar Kunenge amesema mkoa una viwanda 1,453 na 87 viwanda vikubwa na wanaendelea kutumia mikakati mbalimbali ya kuvutia wawekezaji.

About the author

mzalendoeditor