Featured Kitaifa

MAENDELEO YA VIJANA NI KIPAUMBELE CHA RAIS SAMIA-KATAMBI

Written by mzalendo

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (kulia) akizindua rasmi Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana Awamu ya Pili “Safeguard Young People (SYP II)”. Wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Zanzibar, Bw. sahib Mohamed na Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania, Mhe. Didier Chassot (wa pili kutoka kushoto).

Na; Mwandishi Wetu – Dar es Salaam

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amesema Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuyapa kipaumbele masuala ya maendeleo ya vijana nchini. 

Aidha, Mhe. Katambi amesema vijana ni nguvu kazi ya taifa, hivyo kuwezesha kundi hilo kunatoa fursa kubwa ya kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na kuwafanya vijana kuwa chachu kwa maendeleo ya nchi.

Ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana Awamu ya Pili “Safeguard Young People (SYP)” iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Vile vile, Naibu Waziri Katambi amesema serikali imeboresha mwongozo wa utoaji mikopo kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana ambapo kwa sasa mfuko huo unatoa mikopo kwa kijana mmoja mmoja, ambapo maboresho hayo yatawawezesha vijana walio katika sekta isiyo rasmi na wahitimu wa vyuo kujiajiri kwa kuanzisha miradi ya uzalishaji mali.

Kwa upande wengine, Mhe. Katambi amesema programu ya Safeguard Young People ni fursa kwa vijana kujikwamua na changamoto za kijamii na kiuchumi, hivyo amehamasisha ushirikiano katika utekelezaji wa programu hiyo ili kufikia malengo na kuleta mabadiliko chanya kwa vijana.

Naye, Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania, Mhe. Didier Chassot amesema ni wakati wa kutambua mchango wa vijana katika kukuza maendeleo ya taifa. Aidha, ameongeza kuwa serikali ya Uswisi itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza programu hiyo ya SYP kwa lengo la kuwaondolea vijana changamoto za kiafya, kiuchumi, kisaikolojia na kijamii.

Akizungumza mmoja wa wanufaika amesema programu hiyo imewasaidia vijana kujitambu, kijithamini na kuwa na uthubutu katika kufanya maamuzi sahihi.

Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana “Safeguard Young People (SYP)” inalenga kuboresha huduma za afya, elimu ya afya kwa vijana, kuongeza ushirikishwaji wa vijana katika ngazi za maamuzi na pia kuwaunganisha vijana na fursa za kujipatia ujuzi na kipato.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa wa Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana Awamu ya Pili “Safeguard Young People (SYP II)” iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa wa Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana Awamu ya Pili “Safeguard Young People (SYP II)” iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania, Mhe. Didier Chassot akieleza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa wa Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana Awamu ya Pili “Safeguard Young People (SYP II)” iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Tanzania, Mark Shreiner akieleza jambo kuhusu utekelezaji wa Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana Awamu ya Pili “Safeguard Young People (SYP)” wakati wa hafla ya uzinduzi wa programu hiyo jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (kulia) akizindua rasmi Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana Awamu ya Pili “Safeguard Young People (SYP II)”. Wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Zanzibar, Bw. sahib Mohamed na Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania, Mhe. Didier Chassot (wa pili kutoka kushoto).

Mmoja wa Kijana aliyeshiriki tukio la uzinduzi wa Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana Awamu ya Pili “Safeguard Young People (SYP II), Getrude Clement akitoa neno la shukrani wakati wa hafla hiyo.

Wasanii wa muziki wa kizazikipya Ben Pol, Phina na Tommy Flavor wakitoa burudani wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana Awamu ya Pili “Safeguard Young People (SYP II), iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (kushoto) akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Tanzania, Mark Shreiner (kulia). Katikati ni Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania, Mhe. Didier Chassot.

PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

About the author

mzalendo