Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Mkombozi wine kilichopo Mvumi mkoani Dodoma ambao ni wazalishaji wa Mvumi wine Mwanga Chibago amewashukuru wananchi wa mvumi na maeneo ya jirani kwa kuendelea kuwaunga mkono katika kufanikisha kiwanda hicho.
Chibago amesema hayo Jumapili April 7,2024 wakati wa Uzinduzi wa kiwanda hicho ambapo ulihudhuriwa na Viongozi wa Dini, Viongozi wa Kisiasa,Chama na Serikali na wananchi wa mvumi na maeneo ya jirani.
“Kwa namna ya pekee niwashukuru sana wananchi wa mvumi kwa maana wamekuwa wadau wetu wakubwa sana,kiwanda hiki kisingeweza kusimama bila jitihada za wananchi wa tarafa ya Mvumi na Makang’wa hakika isingewezekana”amesema
Aidha amewashukuru SIDO na kusema kuwa watakuwa chini ya SIDO kwa miaka saba wakiendelea kukua.
“Ndugu Mgeni rasmi ilikuwa siyo rahisi kufanya jukumu hili bila kukuita wewe,wewe ndiye uliyekuja kufanya ukaguzi,na wewe ndiye uliyefanya jitihada ili kiwanda hiki kiweze kusajiliwa,na kwa hiyo tunatambua tupo chini ya Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo (SIDO) kwa takribani miaka saba”amesema
Akizingumzia historia fupi ya uanzishwaji wa kiwanda hicho Chibago amesema kuwa Kiwanda cha Mkombozi kimekuwa na ndoto ya muda mrefu kuanzia wazo Mpaka kuwekwa kwenye maandishi na safari ya kiwanda hicho ilianza toka mwaka 2013.
“Tulianza kwa kuandikia andiko kwenda kwenye Bank ya TIB,na katika andiko hilo lilijumuisha mambo mawili ambayo ni kuendeleza shamba la zabibu katika mfumo wa Kilimo cha umwagiliaji na bank ya Kilimo wakati ule ikiitwa Tanzania Investment Bank wakatusapoti kwa milioni 120 tukaendeleza shamba lenye takribani hekali 11″amesema
Pia ameongeza kuwa katika hilo andiko awamu ya Kwanza ilikuwa ni kuendeleza shamba na awamu ya pili ilikuwa ni kufungua kiwanda.
“Taasisi hukua Kama mtu kwa hiyo unaweza kuona katika kipindi hiki kirefu tulikuwa tunakua kupitia hatua mbalimbali,na ilipofika mwaka 2022 tukaendeleza wazo lile na katika Mazingira yale tukawashirikisha bank ya NMB bank ya NMB wakatusapoti kwa fedha za Kutosha walianza kutupatia Milioni 50 na kwa kweli tunawashukuru sana NMB”amesema Chibago
Katika hatua nyingine Chibago amewaomba wananchi wa mvumi kuendelea kupenda kinywaji cha wine kwa sababu wamekuwa wadau wa kweli.
“Lengo kubwa ambalo linatuweka hapa tunataka Mpende kunywa wine,mpende zao la zabibu soko tuwe sisi wenyewe tunakata nani anywe kama sio sisi”amesisitiza Chibago.
Awali Mgeni rasmi kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo (SIDO) Mhandisi Nyangusi Meitalami Kaimu Meneja akizindua kiwanda hicho amesema kuwa Viwanda ni muhimu Sana kwa sababu vinaongeza thamani ya mazao na vinaongeza ajira.
“Kiwanda hiki kimeajili watu zaidi ya Ishirini hizo ni ajira ambazo ni za moja kwa moja,na kuna ajira ambazo sio za moja kwa moja nyingi Sana”amesema
Aidha amesema kuwa Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo (SIDO) ni jukumu lao katika kuhamasisha Viwanda vidogo vidogo na kiwanda cha Mkombozi wine ni kimojawapo.
“Kiwanda kimeanzishwa kwa lengo la kutatua changamoto za wakulima wa zabibu bahati nzuri jina lake kinaitwa Mkombozi basi kiwanda hiki kikawe Mkombozi kwa wananchi wenye zao la zabibu hasa katika eneo hili”amesema
Pia amesema kuwa Kiwanda hicho kihudumie wananchi wote bila kubagua na wale wanaohitaji kwenda kujifunza ili waanzishe Viwanda vingine waruhusiwe kwenda kujifunza.
“Baadhi ya watu wakianzisha Viwanda hawatamani watu wengine waende kujifunza wanaogopa ile changamoto ya ushindani lakini ushindani una ubunifu,bila ushindani hakuna ubunifu”amesema.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mvumi Makulu na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Edison Mdonondo amemuahidi Mkurugenzi wa kiwanda hicho cha Mkombozi Mwanga Chibago Kuwa ataendelea kutoa Ushirikiano kwa kuitangaza Mvumi wine na kiwanda hicho.
“Nipo hapa kama nyie wenzangu wananchi wengine mliofika hapa kwa Mwanga kumuunga mkono na kuondoka tukiwa tunajua kwamba tunaenda kulitangaza soko la hii wine ambayo tumeionja leo hapa”amesema
Pia Mdonondo amesisitiza kuwa bila unafiki,bila wivu kwa sababu mimi Sina kiwanda sitakuonea wivu tunaenda kuitangaza na Mimi kwa nafasi yangu mpaka kwenye Baraza la Madiniwani nitaitangaza
Mdonondo ameongeza kuwa kwa niaba ya Serikali amempongeza Mkurugenzi wa kiwanda hicho Mwanga Chibago na kusema kuwa kama kuna mahali popote panapohisiana na serikali wapo tayari kumsaidia.
“Kwa hiyo kama unaona kuna mahali Mwenyekiti wa Halmashauri ana uwezo wa kukusapoti kwa chochote kupitia Serikali mimi kwa niaba ya Serikali niko tayari kukusaidia”amesema
Aidha amesisitiza kuwa kupitia Wilaya ya Chamwino Mvumi wine itafika kila mahali na watu wataijua
“Mengine haya ni ya kwetu kwa sababu kufika kwangu huku inaweza ikaleta maneno baadae,wanasiasa sisi tunaishi kwa hofo hofu”amesema
Naye Crispin Kapinga Afisa uendelezaji biashara kupitia Shirika la kuhudumia Viwanda vidogo (SIDO) amewaomba wananchi wasijifiche kuzalisha biashara zao na waende SIDO ili waweze kuwasaidia
“Soko lolote linaendeshwa na Private sector serikali inatengeneza Mazingira salama na mazuri japo kuna changamoto za hapa na pale”amesema
Aidha amewahimiza wafabiashara kutumia soko Huru la Afrika Mashariki ili kuweza kutoa bidhaa nje ya Tanzania na kuweza kuwasaidia wakulima kwa sababu Kilimo ndo kimeajili watu wengi
Kwa Upande wake Mkulima wa Zabibu Julius Meshaki kutoka kijiji cha Handali ameiomba Serikali kuwawezesha wamiliki wa Viwanda vidogo vidogo ili waweze kulipa wakulima kwa wakati
Pia ameiomba Serikali iweze kuwaongezea bei kwa sababu bei wanayopewa ni ndogo na Zabibu ina Thamani kubwa,halidhalia Serikali imsaidie kumuwezesha Mkurugenzi wa kiwanda cha Mkombozi Mwanga Chibago kuweza kukipanua zaidi kwa sababu kiwanda hicho kinasaidia wakulima wa zabibu wa maeneo hayo na jirani