Kimataifa

ZAIDI YA WATU 90 WAFARIKI KATIKA AJALI YA MELI MSUMBIJI

Written by mzalendo

Takriban watu 91 wamepoteza maisha baada ya boti iliyokuwa imejazwa mizigo kupita kiasi kupinduka na kuzama karibu na Kisiwa cha Msumbiji katika jimbo la kaskazini mwa Msumbiji la Nampula hapo jana.

Ripoti imesema waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni pamoja na watoto, na watu wengine 34 na na kuongeza kuwa manusura watano tayari wamepatikana.

Mkuu wa Jimbo la Nampula Jaime Neto, amenukuliwa akisema Meli hiyo ilikuwa ikitokea wilaya ya Mossuril ambapo ilikuwa imebeba jumla ya abiria 130.

Neto amesema kuwa abiria waliokuwa katika Meli hiyo walikuwa wamekimbia makazi yao kufuatia hofu iliyosababishwa na habari potofu kuhusu mlipuko wa kipindupindu.

“Ni meli ambayo haijatayarishwa kusafirisha watu wengi. Ni meli ya uvuvi, na watu walikuwa na taarifa potofu kuhusu mlipuko wa kipindupindu, na wakakimbilia kwenye chombo,”amesema Neto.

Jitihada zinaendelea kuwatafuta waliotoweka na kufanya uchunguzi wa ajali hiyo.

About the author

mzalendo