Featured Kitaifa

DCEA KANDA YA KASKAZINI  YAANDAA FUTARI  KWA WARAIBU WANAWAKE JIJINI ARUSHA

Written by mzalendo
Na Prisca Libaga Arusha
Maafisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 07.04.2024 wameshiriki kula futari na Waraibu Wanawake kutoka Nyumba mbili za Upataji Nafuu  za Wanawake zilizopo jijini Arusha ambazo ni Arusha Sober House na Njiro Women Recovery Sober House. 
Lengo likiwa ni kukaa nao pamoja, kuwatia moyo na kujadili  changamoto mbalimbali wanazozipitia kundi hilo pamoja na kuondoa dhana ya unyanyapaa kwa Waraibu wa dawa za kulevya hususani Waraibu Wanawake nchini.
Ofisi ya Mamlaka Kanda ya Kaskazini itaendelea kuyafikia makundi mbalimbali wakiwemo Waraibu wa Jinsia zote katika ukanda wa Mikoa ya Kaskazini kwa lengo tu la kutoa elimu juu tatizo na madhara ya dawa za kulevya pamoja na kubaini changamoto mbalimbali wanazopitia Waraibu hao waliopo katika Nyumba za Upataji Nafuu katika hatua za kuacha kabisa matumizi ya dawa za kulevya na baadaye kuwa watu wema katika jamii zao.

About the author

mzalendo