Featured Kitaifa

MTANZANIA SIMON MNKONDYA APELEKA KILIMO CHA VANILLA KENYA

Written by mzalendoeditor
Mkurugenzi wa Vanilla International Limited wa Tanzania ameweza kufanikiwa kuanzisha mashamba ya Vanilla katika eneo la Kaunti ya Kilith Nchini Kenya ambapo mradi huo mkubwa wa kilimo cha vanilla uko katika mji mdogo wa Mariakani kilomita 40 kutoka jiji la Mombasa.

Mradi huu unafanyika kwa ushirikiano na Mabati Technical Training Institute na wadau wengine wa maendeleo wakiwemo Safaricom Foundation ya nchini Kenya.
 
“Safari ya kilimo cha Vanilla inaenda vizuri licha ya vikwazo vya hapa na pale vya kisiasa lakini kiukweli wakenya wamekipokea kilimo cha vanilla kwa jicho kubwa sana hususani wakenya wanaoishi katika nchi mbalimbali za ughaibuni”, amesema Simon Mnkondya Mkurugenzi wa kampuni ya Vanilla International Limited yenye mashamba yake pia Nchini Tanzania katika eneo la Zanzibar , Arusha na Dodoma.
 
Kwa Upande wa wakenya wamesema mradi huo utakuwa mkombozi wa uchumi wa Kenya na chanzo kikubwa cha ajira na kutoa ahadi ya kuwa watatunza vanilla vizuri na kushukuru kwa elimu ya utunzaji wa vanilla kutoka Mkurugenzi wa kampuni ya Vanilla International Limited Simon Mnkondya (+255 629 300 200).

About the author

mzalendoeditor