Wanawake wawili wameuawa kikatili na watu wasiojulikana katika matukio mawili tofauti mkoani Tabora.
Akithibitisha matukio hayo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao amesema kuwa matukio hayo ya mauaji yalifanyika Jumanne Machi 22, 2022, kati ya saa nane na saa tisa mchana katika Kata ya Malolo Manispaa ya Tabora.
Amewataja marehemu hao kuwa ni Leah Emmanuel ambaye aliuawa nyumbani kwake kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali, huku Safi Simba akihisiwa kunyongwa akiwa shambani kwake.
“Mkazi huyo ameshambuliwa kwa kukatwa katwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake, chanzo cha mauaji haya bado haijajulikana ” amesema Kamanda Abwao
Kamanda Abwao amesema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa mauaji hayo.
Aidha ametoa wito kwa wakazi wa Tabora kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuwabaini wahusika waliofanya tukio hilo.