Featured Kitaifa

MISA YA KUMUOMBEA MAGUFULI YAFANYIKA CHATO

Written by mzalendo

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko pamoja na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa wameungana na familia na waumini kushiriki Misa Takatifu ya kumuombea Rais wa awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Magufuli leo tarehe 17 Machi 2024.

Misa hiyo imefanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Yohana Maria Muzeyi wilayani Chato mkoa wa Geita na kuongozwa na Makamu Askofu, Padri Ovan Mwenge wa Katoke Seminari. 

Padri Mwenge amesema wataendelea kumkumbuka hayati Magufuli kwa yale yote ambayo aliwahi kuyafanya enzi za uhai wake katika kuwatumikia watanzania.

Misa hiyo Takatifu ya kumuombea Rais wa awamu ya Tano Dkt.John Magufuli inafanyika ikiwa imetimia miaka mitatu tangu alipofariki dunia Machi 17, 2021 ambapo imehudhuriwa na Viongozi wa Serikali, familia ikiongozwa na Mke wa Hayati Dkt. Magufuli, Mama Janeth Magufuli, Watoto wa Hayati, Wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki.

About the author

mzalendo