Waombolezaji mbalimbali wameendelea kujitokeza nyumbani Mikocheni kwa Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
Miongoni mwa watu waliofika nyumbani ni Rais mtaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa Wa Dar Albert Chalamila na Viongozi wengine wengi.
Kwa sasa mwili wa hayati Ali Hassan Mwinyi unaswaliwa kwenye msikiti wa Mohamed VI uliopo Kinondoni Jijini Dar es salaam.