Wakongo wakiwa wamebeba mali zao wakikimbia vijiji vyao karibu na Sake, katika eneo la Masisi, kufuatia mapigano kati ya waasi wa M23 na Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC), kuelekea Goma, mkoa wa Kivu Kaskazini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mnamo Februari 7, 2024.
Na Mwandishi Wetu, DRC Congo.
Watu watatu, mama na watoto wake wawili, walifariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa vibaya katika mlipuko wa mabomu yaliyorushwa usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa Februari 23 katika mji wa Sake, katika mkoa waKivu Kaskazini na waasi wa M23.
Kulingana na mashirika ya kiraia ya eneo hilo ambayo yametoa idadi hiyo imesema mapigano makali yaliyotokea tangu usiku wa Alhamisi yaliendelea hadi mapema jana Ijumaa asubuhi ambapo pande zote za jiji la Sake, katika eneo la Masisi ikiwa ni takriban kilomita 27 kusini-mashariki mwa jiji la Goma.
Viongozi wa mashirika ya kiraia katika eneo la Masisi wanathibitisha kwamba shambulio hili jipya la waasi katika jiji hilo lilizuiliwa vikali na jeshi na washirika wake ikiwa ni pamoja na MONUSCO na kikosi cha SADC ambao wanadhibiti mji na viunga vyake.
Vyanzo hivyo pamoja na shuhuda nyingine kadhaa katika eneo hilo, vinabainisha kuwa waasi walijaribu kwa mara nyingine kuzunguka kilima cha Matcha ili kuingia mjini, bila mafanikio.
Hii, baada ya kudondosha mabomu matatu katika jiji hilo. Mashirika ya kiraia yanatoa idadi ya muda ya watu watatu waliouawa, ikiwa ni pamoja na mama na watoto wake wawili katika wilaya ya Mayusa. Wengine wanne walijeruhiwa vibaya, limesema shirika hili.
Mji wa Saké, unaochukuliwa kuwa kitovu cha uchifu wa Bahunde, bado unalengwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya waasi ambao wana nia ya kuuteka mji huu ambao unafungua njia kuelekea mikoa mingine.