Featured Kitaifa

KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DK. NCHIMBI ATUA KAGERA, MAZISHI YA BALOZI DK. DIODORUS KAMALA

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, akipokelewa na kusalimiana na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, alipowasili Uwanja wa Ndege wa Bukoba, mkoani Kagera, leo Jumatatu, Februari 19, 2024, kwa ajili ya kushiriki mazishi ya Balozi (mstaafu) Dk. Deodorus Buberwa Kamala, anayetarajiwa kuzikwa kesho Jumanne, Februari 20, 2024, kijijini kwake Bwanjai, Wilaya ya Misenyi, Mkoa wa Kagera.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, akiwa katika mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali wa Mkoa wa Kagera, baada ya kuwasili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba, mkoani Kagera, leo Jumatatu, Februari 19, 2024, kwa ajili ya kushiriki mazishi ya Balozi (mstaafu) Dk. Deodorus Buberwa Kamala, anayetarajiwa kuzikwa kesho Jumanne, Februari 20, 2024, kijijini kwake Bwanjai, Wilaya ya Misenyi, mkoani humo.


 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, akipokea taarifa kuhusu masuala mbalimbali ya utekelezaji wa Ilani ya CCM y 2020 – 2025, kutoka kwa Viongozi wa Chama na Serikali wa Mkoa wa Kagera, wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Ndugu Nazir Karamagi na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Hajjat Fatma Mwasa na Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato. Balozi Dk. Nchimbi amewasili mkoani Kagera leo Jumatatu, Februari 19, 2024, kwa ajili ya kushiriki mazishi ya Balozi (mstaafu) Dk. Deodorus Buberwa Kamala, anayeratajiwa kuzikwa kesho Jumanne, Februari 20, 2024, kijijini wkake Bwanjai, wilayani Msenyi, Mkoa wa Kagera.

About the author

mzalendoeditor