Featured Kitaifa

SERIKALI KUENDELEA NA UTAFITI WA MAJI ARDHINI

Written by mzalendoeditor

SERIKALI KUENDELEA NA UTAFITI WA MAJI ARDHINI

NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema Serikali inaendelea na zoezi la utafiti wa maji ardhini pamoja na uchimbaji wa visima 13 katika Jimbo la Buchosa Wilayani Sengerema.

Mahundi ameyasema hayo leo Februari 13 2024, bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Buchosa Eric Shigongo aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itakamilisha uchimbaji wa visima vya maji vilivyoanza kuchimbwa katika jimbo la Buchosa.

Mhandisi Mahundi amesema hadi sasa jumla ya visima 6 vimechimbwa, ambapo kati ya visima hivyo vilivyopata maji ni visima 4 vilivyochimbwa katika vijiji vya Bulolo, Nyonga, Bulyahilu na Izindabo.

“Kazi ya utafiti wa maji ardhini na uchimbaji wa visima inaendelea katika Vijiji vya Kisaba, Busikimbi, Kasalaji, Nyamiswi, Luharanyonga, Irenza na Bugoro ambapo unatarajiwa kukamilika Mwezi Juni, 20″amesema Mahundi

About the author

mzalendoeditor