Featured Michezo

BARCELONA YAIFANYIA MAUAJI YA KINYAMA REAL MADRID MCHEZO WA EL CLASICO

Written by mzalendoeditor

Klabu ya Barcelona imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 kwenye mchezo wa El clasico dhidi ya Real Madrid mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu.

Barcelona imefanikiwa kupata mabao kupitia kwa mshambuliaji wao.hatari aliyesajiliwa kutoka klabu.ya Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya  29 na 51,Ronald Araújo dakika ya 38 na Mshambuliaji kinda Ferran Torres dakika ya  47.

Kwa matokeo hayo Real Madrid wanaendelea kuongoza Ligi wakiwa na Pointi 66 wakicheza mechi 29 huku Barcelona wakipanda hadi nafasi ya tatu kwa kufikisha Pointi 54 wakiwa wamecheza mechi 28.

About the author

mzalendoeditor