Featured Kitaifa

WAZIRI MKUU AFUNGUA CHUO KIKUU KATOLIKI MBEYA

Written by mzalendo

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Katoliki Mbeya Prof. Romuald Haule (Kushoto) alipotembelea moja ya Darasa la Mihadhara (Lecture Theatre), wakati wa ufunguzi wa Chuo hicho leo Januari 16, 2024, mkoani Mbeya. Katikati ni Mkuu wa Chuo hicho na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Gervas Nyaisonga. 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Mtaalam wa Mifumo wa Chuo Kikuu cha Katoliki Mbeya Baker Tumaini kuhusu mfumo maalum wa kufundishia kwenye moja ya Darasa chuoni hapo, wakati wa ufunguzi wa Chuo hicho

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Katoliki Mbeya Prof. Romuald Haule wakati alipotembelea Maktaba ya chuoni hapo wakati wa ufunguzi wa Chuo hicho

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa pamoja na maaskofu wa Katoliki, wakuu wa vyuo na viongozi mbalimbali wa Serikali kwenye maandamano ya kitaaluma  wakati wa hafla ya ufunguzi wa Chuo hicho leo Januari 16, 2024, mkoani Mbeya (Picha Na Ofisi ya Waziri Mkuu)

About the author

mzalendo