Featured Kitaifa

DC MSAFIRI AINGILIA KATI MGOGORO WA ARDHI KATI YA MWEKEZAJI KADRI NA WANANCHI WAVAMIZI

Written by mzalendoeditor

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
SERIKALI ya wilaya ya Kibaha, Mkoani Pwani imetoa wiki moja kwa Halmashauri ya Mji wa Kibaha pamoja na Mtendaji kata ya Visiga kupima upya eneo la Mwekezaji KADRI, huko Zegereni -Bwawa la Chumvi ambalo lipo kwenye mgogoro mkubwa na wananchi waliovamia .
Aidha Serikali hiyo, imetoa onyo kwa baadhi ya wananchi na viongozi vinara ambao wanaokuza migogoro ya ardhi kwa maslahi yao binafsi .
Mkuu wa wilaya ya Kibaha,Sara Msafiri alitoa agizo Hilo , wakati alipoingilia kati mgogoro huo baada ya mkurugenzi Mshamu Munde kufumua kamati mbili za wananchi wavamizi waliokuwa wakikinzana kuchelewesha utatuzi wa mgogoro huo .
“Mtendaji wa kata na Mkurugenzi wa Halmashauri mji Kibaha nawapa siku saba muanze zoezi la upimaji ardhi ya mwekezaji ,ikiwa ni mchakato wa kuelekea kutatua mgogoro huu “
“Zoezi litaendelea,na Mwenyekiti wa mtaa atakuwa msimamizi na zoezi litakuwa chini ya vyombo vya ulinzi na Usalama”alisisitiza Sara.
“Mara ya mwisho mliishia mkurugenzi kupanga kamati ya wananchi wa pande mbili za kamati zilizokuwa awali ,tutambue Ni kamati Halali ,kinachotakiwa Ni kufanya utambuzi upya wa ukubwa wa eneo, utambuzi na upimaji wa hekari 250 ambazo mwekezaji anataka kugawa na kujua Kama zitatosha kulingana na watu waliopo ndani toka wavamie ama kuuziwa kinyemeela Hadi mwaka 2017″alisema Sara .
Nae diwani wa Kata ya Visiga Kambi Legeza aliwasihi wananchi hao kuvuta subira na kuiamini Serikali katika zoezi linalokwenda kutatua mgogoro wao.
Kambi alisema, Makubaliano Ni kuwatambua waliouziwa kinyume na taratibu na waliovamia tangu kipindi cha nyuma mwisho 2017 Lakini kufikia 2018 yaliibuka makundi ya kuvamia na wakazi wapya siku Hadi siku na kusababisha mgogoro kuwa mkubwa zaidi.
Awali katibu wa kamati ya wananchi Adam Eliam, alisema kwanza hakuna elimu ya utatuzi wa mgogoro kwa wananchi lengwa.
Alidai hatua iliyopo Ni eneo litambuliwe mipaka ya mwekezaji, kipengele cha pili kutambua hekari alizotoa Mwekezaji, Zina viwanja vingapi,na kutambua wananchi waliopo hadi 2017 .
Mwakilishi wa familia ya mwekezaji KADRI aliyejitambulisha kwa jina la Steve Kadri alisema ,eneo Hilo Lina ukubwa wa hekari 2,800, wanalimiliki kihalali na Ni la kifamilia .
Alieleza, watu waliovamia walikuwa zaidi ya 100 ,na walivyoona eneo linazidi kumegwa wameamua kutoa hekari 250 ili kuondokana na matatizo.

Steve alifafanua, wapo tayari eneo lipimwe na taratibu nyingine zifuatwe kulingana na agizo la Serikali ya wilaya ya Kibaha ,waweze kuendeleza shamba Lao kwa Uhuru .

About the author

mzalendoeditor