MWENYEKITI wa Baraza la wafanyakazi ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.Jaji Dk. Eliezer Feleshi (Kushoto) akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Mohamed Mchengerwa, wakati akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Serikali linalofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Mohamed Mchengerwa,akizungumza leo Desemba 19,2023 wakati akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu serikali linalofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
SEHEMU ya Washiriki wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Mohamed Mchengerwa, wakati akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Serikali kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Baraza la wafanyakazi ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.Jaji Dk. Eliezer Feleshi ,akizungumza wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Serikali kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
NAIBU Mwanasheria Mkuu wa Serikali Balozi, Prof.Kennedy Gaston,akitoa salama za Baraza wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Serikali kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Mohamed Mchengerwa,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Serikali linalofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Mohamed Mchengerwa ,amewataka watumishi wa umma nchini kuwa wazalendo linapokuja suala linalohusu maslahi ya nchi.
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo leo Desemba 19,2023 wakati akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
“Niwapongeze kwa kuwa wazalendo licha ya changamoto mnazokabiliwa nazo katika utumishi wenu hivi sasa watumishi wengi wa umma wamekuwa siyo wazelendo.
“Hata kama kuna jambo litatokea linalohusu kuumiza nchi wao wala haiwagusi, uzalendo ni jambo la msingi lazima kila mmoja wetu awe nalo moyoni”amesema Waziri Mchengerwa
Aidha Waziri Mchengerwa,amemuelekeza Mwanasheria Mkuu wa serikali kukaa na ofisi yake ili kuandaa mpango kazi ambao utasaidia kupata suluhu ya kero mbalimbali.
“Tukae tuandae mpango mkakati ambao utasaidia kutatua changamoto hizi mlizosema kwani TAMISEMI ni ya wananchi hivyo lazima tuweke mazingira mazuri kwa wananchi kupata huduma hizi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali”amesema
Hata hivyo, Mhe.Mchengerwa amesema kuwa tatizo la ukosefu wa vyombo vya usafiri ataifikisha kwa Rais Samia Suluhu Hassan ili kuona ni jinsi gani italifanyia kazi.
Awali Mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.Jaji Dk. Eliezer Feleshi amesema ofisi yake inakabiliwa na upungufu wa watumishi 285 hali inayochangia baadhi ya shughuli kushindwa kutekelezwa kwa ufanisi.
Dk.Feleshi amesema ,mahitaji wa watumishi kwenye ofisi yake ni 477 lakini waliopo hivi sasa ni 192 hivyo kufanya upungufu kuwa ni watumishi 285 katika maeneo mbalimbali.
“Tunaishukuru serikali kwa kutoa kibali cha kuajiri watumishi 50 katika mwaka wa fedha 2022/23 ambapo 48 walikuwa mawakili na wawili ni wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)”amesema Dk. Feleshi
Aidha Dk. Feleshi ameelezea, lengo la kikao hicho cha baraza la wafanyakazi ni kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mpango wa bajeti.
“Pia kupima mafanikio ya mpango wa bajeti, kujadili hoja mbalimbali zitazoibuliwa na wajumbe wa baraza hili na kuzitafutia ufumbuzi”amesema