Featured Kitaifa

CHATANDA AZINDUA KAMATI YA MAPAMBANO DHIDI YA UKATILI WA WANAWAKE NA WATOTO NCHINI

Written by mzalendoeditor

 

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda,akizindua  Kamati ya Mapambano  Dhidi ya Ukatili wa Wanawake na Watoto hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

……..

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda amezindua Kamati ya Mapambano  Dhidi ya Ukatili wa Wanawake na Watoto na kukemea vikali baadhi ya wenza wanaowafanyia Ukatili  Watoto na kuitaka Kamati ya kupinga Ukatili ya UWT kwa  kushirikiana na Wadau wengine kutokomeza Janga Hili Ipasavyo.

Akizungumza    katika Uzinduzi huo katika Mkoa wa Dar es  Salam, Mwenyekiti Chatanda amesema Serikali zote mbili kupitia Wizara zinazoshughulikia Maendeleo ya Jamii pamoja na wadau wanajitahidi  sana kupambana na vita ya Ukatili wa Kijinsia na watoto lakini bado kuna ongezeko kubwa  la ukatili hasa Ulawiti nau Ubakaji ambayo asilimia kubwa uanzia nyumbani, hivyo Niwaombe  Kuchukua hatua  kali kwani Vitendo vingi ufanywa na Wanaume.

Mwenyekiti Chatanda amesema  UWT imeungana na Chuo cha Ustawi wa Jamii kwa  kuadhimisha miaka 50 na  kuzindua Kamati hiyo ikiwa ni wakati muafaka katika kupambana na vitendo vya ukatili wa Kijinsia katika Nchi yetu .

” niwaombe wazazi na walezi Nchini  kuendelea kuwatunza watoto wetu katika maadili  mema na mazuri ili kutokomeza kabisa Janga hili la Ulawiti na Ubakaji kwa watoto wetu .”

Hata hivyo Mwenyekiti Chatanda amesema Kamati hiyo ni miongoni mwa Kamati 7 zilizoundwa na Baraza Kuu la UWT 2022 ikiwa ni moja ya Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan  aliyotaka UWT kushiriki na kujipambanua katika vita dhidi ya ukatili ya wanawake na watoto .

Mwenyekiti Chatanda amesema Takwimu za Shirika la Kimataifa la Wanawake linaonesha kwamba kwenye baadhi ya Nchi Utumia asilimia 2 hadi 3.5 ya bajeti kushughulikia masuala ya ukatili dhidi wanawake na Watoto

Mwenyekiti Chatanda amesema Kamati hii itakuwa chachu ya kuongeza vita dhidi ya Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake na Watoto katika kuendana na dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan , ya kuhakikisha Ukatili sasa basi na Haki na Usawa vinazingatiwa katika Jamii.

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum DKt. Dorothy Gwajima ,amempongeza Mwenyekiti wa Umoja huo Mary Chatanda kwa Maono yake makubwa ya kutengeneza mifumo ya kuhakikisha wananchi wanafikiwa hadi ngazi ya chini na kutatua changamoto zinazowakabili katika Maeneo yao .

Dkt Gwajima amesema  Serikali inaendelea kushirikiana na wadau wote wanaoonesha nia ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia na watoto na kuzinduliwa kwa kamati hii kutaongeza kasi ya utekelezaji wa Afua mbalimbali katika kuisadia Jamii ya Watanzania.

” nikuhakikishi Mwenyekiti wangu wa UWT Taifa sitakuangusha katika kusimamia kikamilifu Kamati hii ambayo tunaaza kwa kasi ya ajabu katika kutoa elimu mbalimbali katika maeneo yote ya Nchi yetu na kwa imani ya mwenyezimungu tutaishinda na watoto watakuwa salama katika Nchi yetu .”

 

About the author

mzalendoeditor