Featured Kitaifa

UVCCM DODOMA WAMPONGEZA RAIS SAMIA

Written by mzalendoeditor

Mwenyekiti wa umoja wa Vijana CCM Mkoa wa Dodoma (UVCCM ),Bill Chidabwa akiongoza wananchama wa UVCCM Dodoma kukagua ujenzi wa soko la kisasa la Machinga Complex linalojengwa eneo la njia panda ya kuelekea Bahi jijini Dodoma ili kujionea maendeleo ya ujenzi huo.

Mwenyekiti wa umoja wa Vijana CCM Mkoa wa Dodoma (UVCCM ),Bill Chidabwa akiongoza wananchama wa UVCCM Dodoma,wakisikiliza Mradi wa ujenzi wa Soko la Wamachinga Complex linalojengwa eneo la njia panda ya kuelekea Bahi jijini Dodoma ili kujionea maendeleo ya ujenzi huo.

Mwenyekiti wa Machinga mkoa wa Dodoma Bruno Mponzi akizungumza na kutoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea Soko la Kisasa na kuendelea kuwajali Wamachinga.

………………………………………………………

Na Bolgas Odilo-DODOMA

Mwenyekiti wa umoja wa Vijana CCM Mkoa wa Dodoma (UVCCM ),Bill Chidabwa
, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassani kwa kuwatengea eneo la kufanyia biashara wamachinga mkoani Dodoma.

Ameyasema hayo mapema leo 16 Machi 2022 jijini Dodoma wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua  ujenzi wa Soko jipya la Machinga Complex lililopo njia panda ya kuelekea Bahi jijini Dodoma ili kujionea maendeleo ya ujenzi huo.

Chidabwa amesema  kuwa, moja ya kiu kubwa ya vijana wa mkoani Dodoma ni kuona wanapata eneo ambalo ni maalumu kwao kwa kufanyia biashara ambapo wanaona kiu hiyo unaenda kutimia.

“Tupo hapa kwa ajili ya kujiridhisha kwa kutembelea mradi mkubwa unaogusa vijana moja kwa moja ambapo eneo hili ni kubwa na pia linapatikana katikati ya mji ambapo tunaamini haijawahi kutokea nchi nzima.

“Tunapenda kumpongeza Rais wetu Mama Samia kwa juhudi anazoendelea kuzifanya katika nchi yetu na kwa kuwajali watu wote kama tunavyoona huu ujenzi unaoendelea hapa hii ni kwaajili ya wafanyabiashara wadogo wadogo tunampongeza sana na uongozi wa mkoa kwa ujumla,” alisema.

Aidha alisema kuwa, moja kati ya vitu ambavyo havijawahi kutokea ni kutengwa kwa eneo kubwa ambalo wamajinga watalitumia kufanyia biashara zao ambapo kwa tanzania nzima Dodoma ndiyo imekua mfano.

”Dodoma ndio imetoa dira nini kifanyike kwa wamachinga ili kutatua matatizo ambayo tunayaona kwa wamachinga wote nchini ambapo moja ya matatizo ni ukosefu wa maeneo ya kufanyia biashara,” alisema Chidabwa

Kwa upande wake, Mhandisi Mkuu wa mradi, Ntezimana Michael alisema mpaka sasa mradi umefikia asilimia 68 na matarajio ni kuukamilisha ndani ya muda uliopangwa .

Naye, Mwenyekiti wa machinga Mkoa wa Dodoma, Bruno Mponzi aliishukuru serikali kwa kuwatengea eneo huku akiiomba kuangalia upya uamuzi wa watu zaidi ya wawili kutumia kizimba kimoja akidai mafahari wawili hawakai zizi moja.

About the author

mzalendoeditor