Featured Kitaifa

TASAC YATAKA WAFANYABIASHARA MPAKANI KUACHA KUTUMIA NJIA ZA PEMBENI KUPITISHA MIFUGO

Written by mzalendoeditor

MWENYEKITI
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Shirika la Meli Tanzania (TASAC)
Captain Mussa Mandia kulia akisisitiza jambo wakati wa ziara yake
mpakani mwa Tanzania na Kenya eneo la Horohoro
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Shirika la
Meli Tanzania (TASAC) Captain Mussa Mandia kulia akisisitiza jambo
wakati wa ziara yake mpakani mwa Tanzania na Kenya eneo la Horohoro
MWENYEKITI
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Shirika la
Meli Tanzania (TASAC) Captain Mussa Mandia kulia akipata maelezo kutoka
kwa Afisa Mfawidhi wa TASAC Mkoa wa Tanga Captain Christopher Shalua
wakati wa ziara yake mpakani mwa Tanzania na Kenya eneo la Horohoro
MWENYEKITI
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Shirika la
Meli Tanzania (TASAC) Captain Mussa Mandia kushoto akimsikiliza kwa
umakini mmoja wa watumishi wanaofanya kazi eneo la mpakani kupitia
wakala huo wakati wa ziara yake mpakani mwa Tanzania na Kenya eneo la
Horohoro

MWENYEKITI
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Shirika la
Meli Tanzania (TASAC) Captain Mussa Mandia aliyekaa katikati
akifuatilia kwa umakini maelezo mbalimbali mara baada ya kufika eneo
hilo la mpaka

Watumishi
kutoka taasisi mbalimbali zinazofanya kazi mpakani mwa Tanzania na
Kenya eneo la Horohoro wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)


NA OSCAR ASSENGA, MKINGA

MWENYEKITI
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Shirika la Meli Tanzania (TASAC)
Captain Mussa Mandia amewataka wafanyabiashara wa mifugo mipakani nchini
kutoa ushirikiano kwa wakala huo huku ikiwataka pia kuacha tabia ya
kutumia njia za pembeni badala yake wapitishe kwenye mpaka huo ili
serikali iweze kupata mapato yake

Captain Mandia aliyasema hayo
leo wakati wa ziara yake kutembelea mpaka huo unaotenganisha kati ya
nchi ya Tanzania na Kenya eneo la Horohoro ili kuweza kujifunza na kuona
shughuli zinazofanyika kwenye maeneo ya mpaka huo.

Akiwa kwenye
mpaka huo aliwatataka wafanyabiashara waongeza ushirikiano ili
kuiwezesha Serikali iweze kukusanya mapato yake ikiwemo kuacha kutumia
njia pembeni kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria

“Kama leo nipo
hapa mpakani wa Kenya na Tanzania eneo Horohoro nimeambiwa usafirishaji
mifugo umepungua sana kutoka 10,000 mpaka 3000 sawa na asilimia 30 ya
mifugo sababu kubwa ni ukwepaji wa kupitisha mifugo kwenye kituo hiki
kwa sababu mbalimbali

Mwenyekiti huyo wa bodi alisema wao kama
Wakala wataliangalia hilo na kujaribu kuboresha mazingira na kuhakikisha
wafanyabiashara wanafaidika na serikali haipotezi mapato.

“Niwaambie
kwamba acheni kutumia njia za pembeni mkiwa na malalamiko yenu
yafikisheni kwetu nasi tutaona namna bora ya kuboresha biashara ya
mifugo hapa mpakani “Alisema Mwenyekiti huyo wa Bodi.

Aidha
alionyeshwa kufurahishwa na hatua ya wakala huo mpakani hapo
kushirikiana vema na mamlaka nyengine zilizopo mpakani na kuweza
kuboresha makusanyo ya kodi ya nchi yetu yameonekana kwa asilimia 500
ndani ya mwaka mmoja.

Alisema hilo ni jambo muhimu na linahitaji
kutazamwa kwa jicho zuri zaidi ili kuweza kuliendeleza na kuongeza wigo
mkubwa zaidi ya ukusanyaji wa mapato ya serikali.

About the author

mzalendoeditor