Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kutokana na upekee wa Bima ya Afya kwa Wote, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha wamependekeza baadhi ya vyanzo vya mapato vya kuendesha mfuko huo.
Vyanzo hivyo ni pamoja na sehemu ya mapato yatokanayo na ushuru wa bidhaa kwenye vinywaji vyenye kaboni, vinywaji vikali,
bidhaa za vipodozi, kodi ya michezo ya kubahatisha, ada ya Bima za vyombo vya moto na mapato yatokanayo na ushuru wa miamala ya kielektroniki kwa kadiri itakavyopendekezwa na Waziri mwenye dhamana na masuala ya fedha, fedha zitakazotengwa na Bunge, mapato yatokanayo na uwekezaji wa mfuko na zawadi
pamoja na misaada kutoka kwa wadau mbalimbali.
Waziri Ummy ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote ambao ulikwama mwezi Februari mwaka huu kwa hoja iliyotolewa na Bunge ya kutokuwepo kwa chanzo endelevu cha fedha za kutekeleza mpango huo.