Uncategorized

BILIONI 23.49 KUJENGA BARABARA ZA LAMI ILEMELA

Written by mzalendo
Kiasi cha shilingi 23,490,253.00  (Bilioni 23.49) kinatarajiwa kutumika kwaajili ya ujenzi wa barabara za Buswelu-Nyamadoke-Nyamhongo yenye urefu wa kilomita 9.5 na barabara ya Buswelu-Busenga-Coca Cola yenye urefu wa kilomita 3.3 ndani ya jimbo la Ilemela
Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela MNEC Mhe Dkt Angeline Mabula katika viwanja vya shule ya msingi Nyamhongolo wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kukagua miradi ya maendeleo ambapo amesema kuwa jimbo la Ilemela lina barabara zenye  jumla ya urefu wa Km 878  huku Km 38.47 pekee zikiwa zimewekwa Lami sawa na 4%, Hivyo kutekelezwa kwa mradi huu wa ujenzi wa barabara kutasaidia kumaliza kero na changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa barabara za uhakika kwa wananchi wa kata ya Nyamhongolo na Ilemela kwa ujumla wake 
‘.. Tunamshukuru sana Rais Mhe  Dkt Samia Suluhu Hasan, Kiukweli tumpe maua yake, ametoa zaidi ya Bilioni 33 kwaajili ya miradi ya maendeleo Ilemela ikiwemo na huu wa barabara na amesema mradi usianze kabla ya kulipa wananchi fidia zao ..’ Alisema 
Aidha Mhe Dkt Mabula ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hasan kwa kumuamini na kumteua kutumikia nafasi ya waziri wa ardhi kwa kipindi chote alichokuwa akiitumikia wizara hiyo pamoja na kumshukuru kwa fedha za maendeleo alizozitoa kwaajili ya miradi mbalimbali ndani ya jimbo lake
Kwa upande wake mstahiki meya wa manispaa ya Ilemela Mhe Renatus Mulunga amesisitiza wananchi kuhakikisha wanalipa kodi za Serikali kwa kuwa kufanya hivyo kutaisaidia Serikali kupata fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo barabara za Lami
Yusuph Ernest Bujiku ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilemela ambapo amesema kuwa anaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo unaofanyika ndani ya wilaya yake sanjari na kuwataka wananchi wa wilaya hiyo kuiunga mkono Serikali na viongozi wake
Dkt Angeline Mabula amepata wasaa wa kukabidhi mifuko ya Saruji 100 kwaajili ya ujenzi wa Zahanati za Bwiru kata ya Pasiansi na Lubala kata ya Kitangiri kila moja ikipata mifuko 50 iliyotolewa na Benki ya (TCB) Tanzania Commercial Bank, kukabidhi hati miliki kwa wananchi wanaopata huduma za Kliniki ya ardhi katika viwanja vya Furahisha, kukagua mradi wa maji Nyamhongolo na kuzungumza na mawakala wa mabasi katika stendi ya Mabasi na Malori Nyamhongolo

About the author

mzalendo