Hivi ndivyo unavyoweza kusema ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni! Ndoa isiyo ya kawaida imefanyika nchini Indonesia – mwanamke mwenye umri wa miaka 70 kaolewa na mvulana wa miaka 16.
Ndoa hii lilidhihirika baada ya video ya harusi yao kusambaa mitandaoni.
Kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya nchi hiyo, ndoa za utotoni haziruhusiwi, lakini wanandoa hao walisema wangejiua ikiwa hawataruhusiwa kuoana, ndio maana mamlaka ya kijiji iliidhinisha ndoa yao lakini haikusajiliwa kwenye daftari la serikali.
CHANZO:BBCSwahiliÂ