Featured Kitaifa

KITUO CHA ELIMU KIDIGITALI CHAZINDULIWA NELSON MANDELA

Written by mzalendoeditor

 

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Professa Ladislaus Mnyone (aliyeshika Mkasi) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa kituo cha Elimu Kidigitali (C-CoDE) katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, kulia ni  Mwakilishi wa Balozi wa Uswissi Nchini Bw.  Holger Tousch na wa Kwanza kushoto ni Dr.Jérôme Chenal kutoka EPFL na wa pili kushoto ni Makamu Mkuu wa Taasisi ya Nelson Mandela Professa Maulilio Kipanyula.

………………..

Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela imezindua rasmi kituo cha Elimu kwa Kidigitali ambacho kitatumiwa na Wahadhiri katika kuandaa vipindi na kufundisha waalimu na wakufunzi kutoka kwenye vyuo mbalimbali nchini kwa ajili ya kuwajengea uwezo.

 

Akizungumza katika hafla za ufunguzi wa kituo hicho leo Oktoba 2,2023 Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Teknolojia Profesa ladislaus Mnyone ameeleza kuwa, Serikali ina shauku kubwa ya kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anapata fursa ya kutosha katika kupata elimu na kituo hicho ni mafanikio makubwa ya kufanikisha azma hiyo.

 

“kituo hiki kitasaidia si tu kuchagiza utoaji wa elimu na kutoa elimu iliyo bora, lakini vilevile itawafanya vijana wetu wapende kujifunza, na hivyo kupata  maarifa na umahiri wa kutosha katika kuleta matokeo chanya kupitia Teknolojia” anasema Profesa Mnyone

 

Ametoa rai kwa wadau mbalimbali nchini kutumia kituo hicho kama fursa ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo ya sekta ya elimu, kwa kuhakikisha vijana wa kitanzania wanafikiwa kwa wingi kwa kupata elimu kutumia digitali.

 

Naye Makamu Mkuu wa Taasisi Profesa Maulilio Kipanyula ameeleza kuwa, ufunguzi wa kituo hicho ni wa kihistoria na taasisi itakuwa ikitoa elimu kidigitali na hivyo kuwezesha watanzania kupata maarifa kwa usawa wakiwa mahali popote nchini na je ya nchi.

 

“Kwa muda mrefu tulikuwa tumenuia kuanzisha kituo hiki cha kutoa elimu kwa njia ya digitali na ukizingatia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilitilia mkazo suala hili nasi tunafurahi kuwa tumefanikisha” Anasema Professa Maulilio.

 

Kwa Upande wake Mwakilishi wa Balozi wa Uswizi nchini Bw. Holger Tausch ameipongeza Taasisi ya Nelson Mandela kwa kufanikisha ufunguzi wa kituo hicho muhimu kwa maendeleo ya sekta ya elimu nchini.

 

Kituo cha Elimu cha Kidigitali (C-CoDE) ni matokeo ya ushirikiano wa vyuo viwili ambavyo ni EPFL na Mohamed wa Sita kutoka nchini Morocco kupitia  Serikali ya Uswizi.

 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Professa Ladislaus Mnyone akizungumza na wajumbe waliohudhuria hafla ya ufunguzi wa kituo cha Elimu Kidigitali (C-CoDE) katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela.

Makamu mkuu wa Taasisi hiyo,Prof Maulilio Kipanyula akizungumza katika uzinduzi huo jijini Arusha 

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Professa Ladislaus Mnyone (aliyeshika Mkasi) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa kituo cha Elimu Kidigitali (C-CoDE) katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, kulia ni  Mwakilishi wa Balozi wa Uswissi Nchini Bw.  Holger Tousch na wa Kwanza kushoto ni Dr.Jérôme Chenal kutoka EPFL na wa pili kushoto ni Makamu Mkuu wa Taasisi ya Nelson Mandela Professa Maulilio Kipanyula.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Professa Ladislaus Mnyone (katikati mwenye tai nyekundu) akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa Masuala ya Habari na Tehama Bw. Octaviani Kanyengere baada ya ufunguzi kituo cha Elimu Kidigitali (C-CoDE) katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela,wengine ni Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilio Kipanyula (kushoto) , Mwakilishi wa Balozi wa Uswissi Nchini Bw.  Holger Tousch (wa pili kushoto) na waliosimama nyuma wa kwanza ni Katibu Tawala Msaidizi Bw. David Lyamongi  na wa pili ni wakilishi kutoka UM6P Dr. Rafiq El Alam.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Professa Ladislaus Mnyone (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe waliohudhuria   ufunguzi wa kituo cha Elimu Kidigitali (C-CoDE) katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela.

About the author

mzalendoeditor