Featured Kitaifa

WATU SABA MATATANI KWA TUHUMA ZA KOSA LA UDANGANYIFU MTIHANI WA DARASA LA SABA MKOANI MWANZA

Written by mzalendoeditor

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limewahoji watu saba kwa tuhuma za kosa la  udanganyifu wa mitihani ya darasa la saba kwa kuwachukua wanafunzi wa sekondari na  kuwafanyisha mitihani hiyo kwa niaba ya wanafunzi wa darasa la saba. 

Tukio hilo lilitokea tarehe 13.09.2023 muda wa saa nane mchana huko katika shule ya  msingi Igulumuki, kata ya Igulumuki, tarafa ya Sengerema wakati kamati ya mitihani  ya wilaya ya Sengerema ilipotembelea shule hiyo kwa ajili ukaguzi na kubaini kufanyika  kwa udanganyifu huo ambapo mkondo namba mbili na namba tatu kulikuwa  kumeingizwa wanafunzi wa sekondari watatu na kufanya mitihani ya darasa la saba. 

Watuhumiwa waliokamatwa na wanaendelea kuhojiwa ni 1.Maiko Sheusi, miaka 35,  mwalimu wa shule ya Sekondari Sima ambaye ni msimamizi mkuu wa mtihani shule  ya msingi Igulumuki 2.Musa mwashihava, miaka 38, mwalimu wa shule ya sekondari  Kilabela ambaye ni msimamizi wa mtihani mkondo namba 2, 3 Bonasi Balozi, miaka  33, mwalimu wa shule ya sekondari Buzilasoga ambaye alikuwa msimamizi wa  mtihani mkondo namba 3, 4 Azizi Mohamed, miaka 36 ,Mwalimu wa taaluma, shule  ya msingi Igulumuki , 5 Shadrack Bwana, miaka 14, mwanafunzi wa shule ya  sekondari Sima, 6 Revocatus Paulo, miaka 14, mwanafunzi wa shule ya sekondari  Sima. 7. Pendo Bukoma, miaka 14, mwanafunzi wa shule ya sekondari Sima, mkazi  wa Igulumuki.  

1 | P a g e 

Kufuatia tukio hilo mwalimu mkuu wa shule ya msingi Igulumuki aitwaye Amlesian  Mahingu Mfungo aliweza kukimbia mpaka sasa Jeshi la Polisi tunaendelea na jitihada  za kumsaka ili aweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria. 

Watuhumiwa wote wamehojiwa kwa kina na watafikishwa mahakamani haraka  iwezekanavyo baada ya upelelezi kukamilika. Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza pamoja  na kutoa elimu, pia limeendelea kuimarisha ulinzi maeneo yote na halitasita kuchukua  hatua kali za kisheria kwa wahalifu. 

Katika tukio lingine, Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linafanya uchunguzi kufuatia  taarifa zilizotolewa kwenye kikao cha kusikiliza kero siku ya tarehe 18.09.2023 kwamba  kampuni iitwayo Alliance Global in Motion ambayo imefungua ofisi yake katika jengo  la Rock City Mall wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza inayojihusisha na vitendo vya  utapeli dhidi ya vijana wakitanzania 150 kwa kuwatoza fedha kwa kigezo cha kufanya  biashara ya tiba lishe kwa njia ya mtandao huku wakiendelea kuwashawishi vijana  wengine kujiunga kwenye biashara hiyo inayodaiwa kuwa ni yautapeli. 

Uchunguzi huo ulianza tarehe 19.09.2023 kufuatia taarifa hizo kutoka kwa wananchi  kwa kuwahoji watu mbalimbali wakiwemo wanachama 46 kati yao mabinti wawili wa  kampuni hiyo kutoka mikoa mbalimbali. Aidha, tumeendelea kufuatilia uhalali wa  kampuni hiyo pamoja na shughuli inazozifanya kwa mujibu wa sheria na katika  uchunguzi huo tutashirikiana kwa ukaribu zaidi na tasisi nyingine za Serikali. 

Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza tunawaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano  kwa kutoa taarifa zitakazosaidia uchunguzi kuhusiana na malalamiko yaliyotolewa.  

Imetolewa na:  

Wilbrod W. Mutafugwa – SACP 

Kamanda wa Polisi  

Mkoa wa Mwanza 

About the author

mzalendoeditor