Featured Kitaifa

WAZIRI NDALICHAKO ARIDHISHWA MAANDALIZI YA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2023

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati)  akikagua miundombinu ya uwanja wa kwaraa patakapo fanyika maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge wa uhuru 2023 Mkoani Manyara, kulia kwake ni Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar,Fatma Hamad Rajab.

Na. Mwandishi wetu Manyara

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema ameridhishwa na maandalizi ya shughuli za kilele cha mbio za mwenge wa uhuru 2023 Mkoani Manyara.

Prof. Ndalichako amesema hayo Mkoani humo alipofanya ziara kwa ajili ya kukagua maendeleo ya shughuli za kilele hicho zitakazofanyika Oktoba 14, 2023.

Aidha ameutaka uongozi wa mkoa huo kukamilisha ujenzi wa uwanja wa kwaraa kabla ama ifikapo Septemba 30, 2023.

Amempongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha zaidi ya shilingi Milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja huo na miundombinu nyingine.

Prof. Ndalichako ametoa wito kwa watanzania hususan mikoa ya Jirani kujitokeza kushiriki katika maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge wa uhuru ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha, amekagua uwanja wa kwaraa yatakapofanyika maadhimisho hayo, Kanisa la Parokia Mtakatifu itakapo fanyika ibada ya Baba wa Taifa, uwanja wa stendi ya zamani itakapo fanyika wiki ya vijana na kukagua maendeleo ya vijana wa halaiki.

Waziri Ndalichako katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar,Fatma Hamad Rajab.

Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2023 zinaongozwa na kauli mbiu isemayo “Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa ustawi wa viumbe hai na Uchumi wa Taifa”.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Fatma Hamad Rajab ameupongeza Uongozi wa Mkoa huo Kwa jitihada wanazozifanya katika kujenga uwanja huo.

Sambamba na hayo amewasihi kuendeleza ushirikiano ili kuhakikisha ujenzi unamilika kwa wakati.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa tatu kushoto)  akikagua uwanja wa stendi ya zamani itakapo fanyika wiki ya vijana Mkoani Manyara.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa tatu kushoto) akikagua Kanisa la Parokia Mtakatifu itakapo fanyika ibada ya Baba wa Taifa Mkoani Manyara

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa kwanza kushoto)  akikagua uwanja wa kwaraa yatakapofanyika maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge wa uhuru 2023 Mkoani Manyara.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati)  akikagua miundombinu ya uwanja wa kwaraa patakapo fanyika maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge wa uhuru 2023 Mkoani Manyara, kulia kwake ni Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar,Fatma Hamad Rajab.

Vijana wa halaiki watakao shiriki katika siku ya kilele cha mbio za mwenge wa uhuru 2023 Mkoani Manyara.

Muonekano wa uwanja wa Kwaraa ambao unatarajiwa kukamilika Septemba 30, 2023 kwa ajili shughuli za kilele cha mbio za mwenge wa uhuru Mkoani Manyara.

About the author

mzalendoeditor