WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. George Simbachawene,akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 24,2023 mara baada ya kufanya ziara yake ya kukagua nyumba 1000 za watumishi wa Umma zilizopo Kisasa na Ndejengwa jijini Dodoma zinazojengwa na Watumishi Housing.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. George Simbachawene,akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investment(WHI), Dk. Fred Msemwa kabla ya kuanza ziara yake ya kukagua nyumba 1000 za watumishi wa Umma zilizopo Kisasa na Ndejengwa jijini Dodoma zinazojengwa na Watumishi Housing ziara iliyofanyika leo Agosti 24,2023.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. George Simbachawene,Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora ,Ridhiwani Kikwete wakikagua nyumba 1000 za watumishi wa Umma zilizopo Kisasa na Ndejengwa jijini Dodoma zinazojengwa na Watumishi Housing ziara iliyofanyika leo Agosti 24,2023.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. George Simbachawene,akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investment(WHI), Dk. Fred Msemwa wakati wa ziara ya kukagua nyumba 1000 za watumishi wa Umma zilizopo Kisasa na Ndejengwa jijini Dodoma zinazojengwa na Watumishi Housing ziara iliyofanyika leo Agosti 24,2023.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akimuonyesha Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Dkt. Fred Msemwa namna alivyovutiwa na mojawapo ya nyumba zilizojengwa na Watumishi Housing Investments (WHI) walipokuwa wakimsubiri Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kukagua mradi wa nyumba hizo eneo la Kisasa Relini jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. George Simbachawene,akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 24,2023 mara baada ya kufanya ziara yake ya kukagua nyumba 1000 za watumishi wa Umma zilizopo Kisasa na Ndejengwa jijini Dodoma zinazojengwa na Watumishi Housing.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kukagua mradi wa nyumba zilizojengwa na Watumishi Housing Investments (WHI) eneo la Njedengwa na Kisasa Relini jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa WHI.
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investment(WHI), Dk. Fred Msemwa ,akimshukuru Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. George Simbachawene,mara baada ya kukagua nyumba 1000 za watumishi wa Umma zilizopo Kisasa na Ndejengwa jijini Dodoma zinazojengwa na Watumishi Housing ziara iliyofanyika leo Agosti 24,2023.
Muonekano wa nyumba zilizojengwa na Watumishi Housing Investments (WHI)
Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. George Simbachawene ameipongeza Watumishi Housing Investments (WHI) kwa kujenga nyumba za gharama nafuu nchini kwa ajili ya kuwauzia na kuwapangisha watumishi wa umma huku akiwasisitizia kuwauzia watumishi ambao ni vijana na wanaoanza maisha.
Pongezi hizo amezitoa leo Agosti 24,2023 wakati wa ziara yake ya kukagua nyumba 1000 za watumishi wa Umma zilizopo Kisasa na Ndejengwa jijini Dodoma zinazojengwa na Watumishi Housing.
Waziri Simbachawene amesema utekelezaji wa nyumba bora za watumishi huo ni mwelekeo mzuri katika kutekeleza sera ya makazi kwa watumishi wa Umma inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita lakini pia imeelezwa katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Katika hili kwa kweli nawapongeza sana kwa sababu mmefanya vizuri hongereni sana,Dar es salaam,Morogoro na Mwanza mmefanya hivyo.
“Lakini pia mnaendelea na miradi mipya endeleeni kuhakikisha watumishi wetu hapa nchini wanapata makazi karibu na maeneo yao wanayofanyia kazi,”amesema Waziri Simbachawene.
Aidha,Waziri Simbachawene amewapongeza wateja wanaonunua nyumba zinazojengwa na Watumishi Housing ambapo nyingi ni Taasisi za Umma na Watumishi wa Umma.
“Na hapa ndipo ninapotaka nitie msisitizo kwamba watumishi tunawaolenga ni wale wanaoanza kazi ama ambao wameenda katika maeneo ambayo hawana nyumba,”amesema Simbachawene.
Amesema nyumba hizo zisilengwe kuwauzia watumishi kwa sababu ya nafasi zao au ya uwezo wao ilenge kuwashawishi hata wale ambao hawana uwezo wa kujenga nyumba.
Amesema wapo baadhi ya vijana ndio wanaanza kazi badala ya kufikiria kutafuta kiwanja na fundi inakuwa ngumu hivyo nyumba hizi zilenge pia kwa vijana hao.
“Nyumba kama hii inamtosha kabisa kijana anaeanza maisha lakini ukimwambia aanze kutafuta kiwanja na urasimu huko tunapoteza watu wengi elimu ipelekwe hasa kwa watumishi wanaoanza kazi,”amesema Waziri Simbachawene.
Pia amesisitiza kujenga Majengo katikati ya miji ili kuwasaidia wafanyakazi na kuwapunguzi gharama za usafiri.
Katika hatua nyingine,Waziri huyo ameagiza wale walionunua nyumba lakini hawajakabidhiwa hati,Shirika hilo wafanye mchakato kuhakikisha walionunua wanapatiwa hati zao.
Vilevile ametaka mikataba ya upangishaji na ununuaji iangaliwe isiwe ya kumkomoa mtumishi.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora ,Ridhiwani Kikwete amesema kazi inayofanywa na Watumishi Housing ni nzuri na Serikali inajivunia uwepo wao.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investment(WHI), Dk. Fred Msemwa amesema
hadi sasa wameweza kutengeneza nyumba 203 ambazo Waziri na Naibu Waziri wamepata nafasi ya kuziona.
Amesema katika nyumba hizo asilimia 99 zimeishauzwa kwa watumishi wa umma ikiwa na maana nyumba 2 pekee ndizo bado hazijauzwa lakini zinaweza kuuzwa wakati wowote kutoka sasa.
“Mimi nichukue nafasi hii kusema kwamba sisi kama WHI tutaendelea kufanya vizuri huku tukizingatia maelekezo ili utekelezaji wa Mpango wa makazi kwa watumishi wa Umma uende vizuri na watumishi zaidi waweze kunufaika na huduma hiii nayotolewa na Serikali.
“Lengo ni watumishi waweze kufanya kazi katika mazingira bora na salama ambayo yatawahakikishia ufanisi na utulivu katika kuwatumikia watanzania katika sekta mbalimbali ambazo wanazohudumu,”amesema Dkt.Msemwa