Featured Kitaifa

RC KINDAMBA AFUNGUA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MATOKEA YA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022

Written by mzalendoeditor

MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza wakati akifungua mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya Watu na makazi yam waka 2022 kwa viongozi, watendaji, wawakilishi na viongozi wa vyama vya siasa mkoani humo ikiwemo makundi maalumu kwa Halmashauri za mkoa huo .

Mratibu wa Sensa Mkoa wa Tanga Tony Mwanjota akizungumza wakati  wa  mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya Watu na makazi yam waka 2022 kwa viongozi, watendaji, wawakilishi na viongozi wa vyama vya siasa mkoani humo ikiwemo makundi maalumu kwa Halmashauri za mkoa huo .

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akizungumza wakati wa mafunzo hayo

MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba katikati akiwa meza kuu na viongozi wengine kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akifuatiwa na Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shilloo

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo kulia akiwa na washiriki wengine wakifiuatilia kwa umakini hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo kulia akiwa na washiriki wengine wakifiuatilia kwa umakini hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba

Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga wakiwa kwenye mafunzo hayo

Washiriki wa mafunzo hayo


Na Oscar Assenga,TANGA

MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amefungua mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya Watu na makazi yam waka 2022 kwa viongozi, watendaji, wawakilishi na viongozi wa vyama vya siasa mkoani humo ikiwemo makundi maalumu kwa Halmashauri za mkoa huo .

huku akieleza kuwa yatawajengea uwezo wakufunzi kuchambua na kutumia matokeo ya sensa ili yawe mwanzo wa dira ya kuwaongoza katika utekelezaji wa majukumu na malengo yao ya kila siku.

Kindamba aliyasema hayo wakati akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Regail Naivera Jijini Tanga ambapo alisema mafunzo haya yatawajengea uwezo wa kutafsiri, kwahiyo nawaomba sana wakati mafunzo yakiendelea kuwa watulivu, ili yaweze kwenda kuwa msaada kwenye ngazi ya chini.

Alisema kwa mujibu wa takwimu ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 idadi ya watu Mkoa wa Tanga idadi imeongezeka lakini siyo kwa idadi kubwa ya watu tofauti na Mikoa mingine Kitaifa.

Aidha alisema Idadi hiyo inaonesha kwamba kiwango cha kuongezeka kimetoka asilimia 2.2 mwaka 2012 na kufikia asilimia 2.5 2022, lakini pamoja na hayo, Mkoa wa Tanga inaonesha kwamba kasi yetu ya kukua iko chini sana ikilinganishwa na takwimu za sensa za Kitaifa ambazo sasa ipo asilimia 3.2.


Katika hatua nyengine Mkuu huyo wa Mkoa alitoa wito kwa viongozi wa halmashauri kuwa makini katika kuhakikisha wanaweka mikakati madhubuti na endelevu itakayowahakikishia wananchi huduma bora na za kiuchumi ili kuimarisha ustawi wao na maendeleo ya Mkoa.

Hata hivyo alisema ni muhimu kutambua Mkoa huo umefunguka kutokana na uwepo wa fursa mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo mradi mkubwa wa bomba la mafuta nao utakuja na watu wake hivyo wao wameamua Tanga iwe kituo cha kuvutia watu waje na hivyo wanapokuja na wenyeji nao wapo.

Awali akizungumza katika mafunzo hayo Meneja wa Takwimu Mkoa wa Tanga Tonny Mwanjota alisisitiza umuhimu wa wadau wa sensa na wananchi kwa ujumla kuwa wavumilivu kwa baadhi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, kusubiria majibu ya matokeo kwa upande wa watu wenye hali ya ulemavu.

Mwanjota amesema matokeo ya sensa bado yanaendelea kutolewa kwa awamu hivyo kwa ugumu wa takwimu kwa wenye ulemavu hivyo nayo yapo miongoni mwa yale ambayo yanaendelea kufanyiwa kazi.

About the author

mzalendoeditor