Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AWAPANGIA VITUO VYA KAZI MABALOZI WATATU NA AMBADILISHIA KITUO CHA KAZI BALOZI MMOJA

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewapangia vituo vya kazi Mabalozi watatu (03) na amembadilishia kituo cha kazi Balozi mmoja (01) kama ifuatavyo:

Mabalozi waliopangiwa vituo vya kazi:

  1. Balozi Khamis Mussa Omar kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini China. Bw. Omar anachukua  nafasi ya Balozi Mbelwa Brighton Kairuki ambaye amehamishiwa London, Uingereza.

2.Balozi Ceaser Chacha Waitara kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Namibia. Bw. Waitara anachukua nafasi ya Balozi Dkt. Modestus Kipilimba ambaye amestaafu. 

3.Balozi Dkt. Benard Yohana Kibesse kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya. Balozi Kibesse anachukua nafasi ya Balozi Dkt. John Stephen Simbachawene ambaye amehamishiwa Kampala, Uganda.

Balozi aliyehamishiwa kituo:

  1. Balozi Mbelwa Brighton Kairuki Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Uingereza. Balozi Kairuki anachukua nafasi ya Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro ambaye amemaliza mkataba wake.

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

About the author

mzalendoeditor