Featured Kitaifa

MAAFISA UGANI WATAKIWA KUTEKELEZA AGENDA YA 10/30 KUINUA KILIMO

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akipata maelezo kutoka kwa Mwanakikundi cha Wanawake ‘Mathabita’ Kiwanja cha Ndege kilichopo jijini Dodoma ambacho kilipata mkopo wa asilimia 10 kwa ajili ya kujishughulisha na ukamuaji wa alizeti na usindikaji wa mazao ya nafaka.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akipata maelezo ya bidhaa zinazozalishwa na Kikundi cha Wanawake ‘Mathabita’ Kiwanja cha Ndege kilichopo jijini Dodoma ambacho kilipata mkopo wa asilimia 10 kwa ajili ya kujishughulisha na ukamuaji wa alizeti na usindikaji wa mazao ya nafaka.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la kikundi cha vijana kilichopo Jijini Dodoma kinachojishughulisha utengenezaji wa viatu ambacho kilipata mkopo wa asilimia 10.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akitumia teknolojia ya nishati safi na nafuu ya kupikia mara baada ya kuitembelea taasisi ya TATEDO katika Maonesho ya Wakulima Nanenane Kanda ya Kati Jijini Dodoma ambayo imebuni teknolojia hiyo inayotumia umeme na gesi kwa lengo la kutunza mazingira.

Na OR-TAMISEMI, Dodoma

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka Maafisa Ugani nchini kuitekeleza Agenda ya 10/30 na kufanyia kazi takwimu za kilimo ili kuwainua wakulima nchini.

Mhe. Ndejembi ametoa malekekezo hayo kwa wagani, alipotembelea taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwenye Maonesho ya Wakulima Nanenane Kanda ya Kati jijini Dodoma na kuwasisitiza kuiunga mkono Wizara ya Kilimo katika kutekeleza Agenda ya 10/30 ya Serikali inayolenga kuwainua wakulima na kilimo ili kukuza Sekta ya Kilimo nchini kwa asilimia 10. 

“Wagani ndio chachu ya kukuza kilimo kwani mnawafikia wakulima walio hadi ngazi ya chini, hivyo muache kufanya kazi kwa mazoea ili kuiwezesha Serikali kuboresha kilimo nchini,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Aidha, Ndejembi ametaka Maafisa Ugani kutumia takwimu za kilimo kuanisha matokeo na mwelekeo wa sura ya kilimo nchini ili kufanya tathmini na tafiti zitakazokuwa na tija kwa wakulima na maendeleo ya kilimo katika Taifa. 

Katika hatua nyingine Mhe. Ndejembi ametembelea vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu waliopata mikopo ya asilimia 10 kupitia Halmashauri na kujionea bidhaa wanazozalisha ambazo zinawawezesha kuirejesha mikopo hiyo ili vikundi vingine vinufaike na mkopo huo. 

Sanjari na hilo, Mhe. Ndejembi alitembelea banda la Ofisi ya Rais- TAMISEMI na kuwataka maafisa walio katika banda hilo kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kwani TAMISEMI ndio inagusa maisha ya watanzania kwa kiasi kikubwa.

Kauli Mbiu ya Maonesho ya Nanenane ya mwaka huu ni “Vijana na wanawake ni Msingi imara wa Mifumo Endelevu ya hakula”.

About the author

mzalendoeditor