Featured Kitaifa

MNKONDYA AFANYA ZIARA KUTEMBELEA MASHAMBA YA VANILLA….. “DAR ES SALAAM NI ENEO SALAMA KWA KILIMO CHA VANILLA”

Written by mzalendoeditor

 

Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited na Vanilla Village Dubai, Simon Mnkondya amesema kuwa, Dar es Salaam ni mahali sahihi kwa kilimo cha zao la Vanilla na kuomba wadau kujitokeza kuwekeza zaidi katika maeneo yao, ikiwemo na maeneo ya Pwani.
Mnkondya amesema hayo wakati alipotembelea shamba la Vanilla lililopo Kunduchi, Dar es Salaam  ambapo shamba hilo na mengine yameanza kufanya vizuri ikiwa ni mwaka mmoja tangu kupandwa kwake.
“Nimetembelea Shamba la Vanilla Kunduchi Dar es Salaam nimeridhika na maendeleo mazuri ya Vanilla kwani limeanza kuzaa. Hii ni habari njema kwa wadau kuchangamkia zao hili. Pia mbali na shamba hilo, Dar es Salaam mashamba 90 yote yanafanya vizuri na Vanilla imeanza kuzaa hivyo kuonekana kuwa, Dar  es Salaam ni mahali salama na sahihi kwa kilimo hiki”, amesema Mnkondya. 
Aidha, ametaja mashamba mengine yaliyopo Dar es Salaam mbali na Kunduchi, pia yapo ya Ununio, Bunju, Boko California, Ubungo Msewe, Kigamboni na mengine mengi kama Bagamoyo, Mkuranga, Kibaha  na mengine.
Aidha, amesema kuwa kwa sasa shamba jipya la Vanilla Village Dodoma limechimbiwa visima virefu vya maji tayari.
“Licha ya ziara, kwenye mashamba yote yanafanya vizuri kwa zaidi ya asilimia 80. Shamba jipya la Vanilla Village Dodoma limechimbwa visima virefu tayari na upandaji wa Vanilla kwa njia ya Vitalu ikiwa ni mashamba Vitalu huku ikifungwa mifumo ya Umwagiliaji wa matone na umwagiliaji wa bunduki”,ameeleza.
Mnkondya amewashukuru Watanzania kwa kuiamini kampuni hiyo, huku akiomba wenye kuhitaji kujifunza bure wamtafute kuwasaidia kupata zao hilo.
“Kwa Watanzania wenye kuhitaji kujifunza watembelee mitandao yetu ya kijamii ama kupitia namba hii 0629300200 ni bure”, amesema Mnkondya. 

 

 

Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited na Vanilla Village Dubai, Simon Mnkondya akiwa katika maandalizi ya Shamba la Vanilla Village Dodoma hivi karibuni
Maandalizi ya mifumo ya upatikanaji wa maji wa visima virefu ukiendelea katika mradi wa shamba la Vanilla Village Dodoma.

 

About the author

mzalendoeditor