Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo,akizungumza wakati wa Kikao kazi cha kujadili usimamizi ya utafiti na maendeleo nchini kilichofanyika leo Julai 31,2023 Mjini Morogoro.
Na.Mwandishi Wetu-MOROGORO
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo ameitaka Tume ya ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kuwa na mfumo mathubuti wa kuratibu tafiti utakaosomana na Taasisi nyingine zinazofanya tafiti.
Agizo hilo Julai 31, 2023 mjini Morogoro katika Kikao kazi cha kujadili usimamizi ya utafiti na maendeleo nchini ambapoa amesema ili kutekeleza hilo kwa ufanisi wizara itaunda kamati ndogo shirikishi ambayo itapitia maoni ya kikao kazi na kuangalia sheria mbalimbali za taasisi zinazohusu masuala ya tafiti ili kutoa mapendekezo.
“Utafiti ni muhimu kwa maendeleo ni vyema ukaratibiwa vizuri ili kupunguza milolongo ya kupatika kwa vibali vya kufanya utafiti na kuwezesha upatikanaji wa matokeo kwa urahisi” amesisitiza Prof. Nombo.
Katibu Mkuu huyo ameongezea kuwa no muhimu kwa taasisi mabimbli kujikita katika kufanya tafiti za pamoja ilinkuleta tija, lakini pia kuhakikisha zinatenga fedha kwa ajili ya tafiti
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Prof. Maulilo Kipanyulu amesema kuwa kikao kazi hicho kinafanyika kwa kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ina jukumu la kutunga na kusimamia utekelezaji wa Sheria na Miongozi ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Utafiti
Naye Mshiriki wa Kikao hicho Makumu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Lughano Kusiluka ameiponeza wizara kwa kikao hicho na kutaka kifanyike mara kwa mara ili kujadili vipaumbele, utekelezaji na matokeo ya tafiti katika maendeleo