Sightsavers Tanzania Inatekeleza mradi wa uwezeshaji kiuchumi kwa watu wenye Ulemavu, Lengo ni kujenga fursa sawa katika upatikanaji wa ajira na kujiajiri kwa watu wenye ulemavu.
Mradi unakusudia kuboresha ujuzi wa wahitimu wenye ulemavu kutoka vyuo vya ufundi stadi,vyuo vikuu na vyuo vya kawaida wenye taaluma na wafanyabishara wenye ulemavu ili kuwajengea ushindaji kwenye soko la ajira, fursa mbalimbali zitakozotolewa ni pamoja na mafunzo ya nadharia na vitendo.
Je, wewe una ulemavu wa aina yeyote? Je unatafuta ajira au unataka kuboresha biashara yako? Tafadhali jiunge kupitia link hii https://forms.office.com/e/y31V0qPuHY ili uweze kutuma maombi ya kuwa mshiriki katika mradi huu.