Katibu Mkuu Prof.Riziki Shemdoe (wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na timu ya wataalam kutoka Tanzania na Ireland wakiendelea na Majadiliano ya namna ya kuboresha Tasnia ya Maziwa Nchini Tanzania.
Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Riziki Shemdoe (wa tano kutoka kushoto) na Bi.Sinead Mcphillips Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kikimo, Chakula na Maliasilia Bahari ya Nchini Ireland (wa Sita kutoka kulia
Na.Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe ameongoza timu ya wataalam kutoka nchini Tanzania unaotembelea nchi ya Ireland kuanzia Tarehe 03.07.2023 kwa ajili ya mashirikiano ya namna ya kuboresha Sekta ndogo ya Maziwa Nchini Tanzania Kwa fedha za msaada wa Serikali ya Ireland.
Aidha, wamefanya majadiliano na wenyeji wao wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Maliasili Bahahari, Bi. Sinéad McPhillips, juu ya namna bora ya Serikali ya Ireland na Serikali ya Tanzania zitakavyoweza kushirikiana katika ukuzaji wa sekta ndogo ya Maziwa Nchini Tanzania.
Pia, Serikali ya Ireland imeipatia Tanzania kiasi cha Euro Milioni Tatu (3m Euros) ambazo ni sawa na taktibalibani Tsh.7.9b kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika taasisi yake ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) ili kuhakikisha tija ya shughuli mbalimbali za utafiti na maendeleo ya Sekta ndogo ya Maziwa kwa kushirikiana na Taasisi inayosimamia “Mamlaka ya Chakula na Maendeleo ya Ireland (TEAGASC)” inapatikana.
Halikadhalika, shughuli za mradi huo ni pamoja na kufanya tafiti, kuendeleza malisho na Ng’ombe bora, kuboresha miundombinu, upatikana wa vitendea kazi na kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wapatao 3,000 kwenye mnyororo wa thamani wa maziwa, hususani watafiti, Maafisa Ugani, vyama vya ushirika na wafugaji wa ng’ombe wa maziwa kwa kuanzia na Mkoa wa Tanga.