Featured Kitaifa

WAZAZI WATAKIWA KUWA KARIBU NA WATOTO WAO.

Written by mzalendoeditor

Wazazi na walezi wametakiwa kuzungumza na watoto wao na kufuatilia mienendo yao kila mara ili kuwaepusha na viendo vya ukatili ikiwa ni Pamoja,ubakaji, ulawiti, mimba za utotoni, kuimarisha upatikanaji wa haki na ulinzi wa Mtoto.

Takwimu zilizotolewa na jeshi la polisi za Januari hadi Disemba 2022 zinaonyesha kuwa jumla ya matukio 12,163 ikiwa na wavulana 2,201 na wasichana 9,962 ukilinganisha na matukio 11,499 kwa mwaka 2021 sawa na ongezeko la matukio 664 (asilimia 5.8)

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Tarafa Farkwa Mathias Kasuga Juni 16, 2023 wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika pamoja na ugawaji wa Vifaa vya shule kwa wanafunzi 150 yalifanyika katika Kijiji cha Rofati , Kata ya Gwandi Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma yaliyoratibiwa na Dorcas Aid Tanzania Pamoja na Tunajali Development Initiativies kwa kushirikiana na Vituo vya Maendeleo ya Mtoto na Vijana Wilaya ya Chemba.

Kasuga amesema watoto bado wanakabiliwa na Changamoto ya vitendo vya ukatili wa aina mbalimbali ikiwa ni Pamoja ulawiti,ubakaji utumikishwaji katika ajira hatarishi, ndoa na mimba za utotoni na kuwataka wazazi/Walezi kutoruhuu mtoto Kwenda kwenye maeneo ambayo ni hatarishi kwa usalama wake.

‘’Vitendo hivyo vinaweza kumshawishi kufanya ngono au kubakwa , kulawitiwa n ahata kuuwawa, pia watoto waheshimu wazazi, walezi, na jamii, kufanya kazi na kutii maelekezo wanayopewa ili kuwasalama kwa ustawina maendeleo yao,’’ amesema Kasuga.

Akizungumzia kauli mbiu katika Maadhimisho hayo ‘’Zingatia Usalama wa Mtoto katika ulimwengu wa Kidigital’’Mratibu wa miradi ya watoto na Wazee kutoka Dorcas Aid Tanzania Pamoja na Tunajali Development Initiativies Goodluck Kivuyo amesema waliamuwa kutumia kauli mbiu hiyo ili kuwakumbusha Wazazi kutumia Digital bila kuathiri malezi ya watoto.

‘’ Unakuta mtoto anaangalia filamu mzazi hafatilii ile filamu ina maudhui gani hivyo kama wazazi watoe elimu kuhusu matumizi sahihi ya mitandao , na mtoto apewe uhuru ili kuweza kufanya maamuzi Pamoja na kujengewa uwezo ili kuelewa athari za mitandao,’’ ameongeza Kivuyo.

Akisoma risala katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika mwanafunzi wa Darasa la Saba wa Shule ya msingi Rofati Sarah Mathew amewataka Viongozi wa dini kutoa elimu ya malenzi ya Ndoa kwa wanandoa ili kupunguza migogoro inayopelekea kushindwa kulea watoto.

Mratibu wa Kituo cha maendeleo ya mtoto na kijana Kijiji cha Rofati Wilaya ya Chemba Ombeni Sifaeli amewataka wazazi kutoruhusu mtoto kutumia vifaa vya kielektroniki kama simu, intaneti, na luninga ungalizi wa karibu ili kumuepusha kujiingiza kwenye maeneo hatari ya kuweza kufanyiwa ukatili wa mitandaoni.

Chimbuko la maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ni tukio la mauaji ya watoto takribani 2,000 yaliyofanywa na Askari wa Utawala wa Makaburu katika Kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini tarehe 16 Juni, 1976. Mauaji hayo yalitokea wakati Askari hao wanazuia maandamano ya watoto waliokuwa wanapinga mfumo wa elimu ya kibaguzi iliyokuwa inatolewa na Utawala wa Makaburu. Katika kukumbuka siku hii, Umoja wa Nchi za Afrika mnamo mwaka 1991 uliweka Azimio la kuifanya siku ya tarehe 16 Juni ya kila mwaka kuwa siku maalum ya kuwaenzi mashujaa watoto waliokufa kwa ajili ya kudai haki yao ya kuendelezwa kielimu bila ubaguzi.

About the author

mzalendoeditor