Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI TENA

Written by mzalendoeditor

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewateua wafuatao:

i.Amemteua Bw. Tito Philemon Mganwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe; na

ii.Amemteua Bw. Mussa R. Kilakala kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kaliua Mkoa wa Tabora.

2.Aidha, Mhe. Rais amefanya mabadiliko madogo ya vituo vya kazi kama ifuatavyo:-

i.Bw. Athumani Francis Msabila kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga;

ii.Bi. Mwantum Hamis Mgonja kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji; na

iii.Bi. Mwamvua Bakari Mnyongo kutoka Wilaya ya Kaliua Mkoa wa Tabora kwenda kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Chemba, Mkoa wa Dodoma.

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

About the author

mzalendoeditor