Featured Kitaifa

MAWAKILI WA SERIKALI WATAKIWA KUTATUA MIGOGORO KWA NJIA YA MAJADILIANO NA USULUHISHI NCHINI

Written by mzalendoeditor
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi.Mary Makondo,akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa Mawakili wa Serikali yaliyokwenda sambamba na Maadhimisho ya miaka Mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali yaliyokuwa na kauli mbiu isemayo “Miaka mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Tulipotoka,Tulipo na Tunapokwenda” 
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende,akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa Mawakili wa Serikali yaliyokwenda sambamba na Maadhimisho ya miaka Mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali yaliyokuwa na kauli mbiu isemayo “Miaka mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Tulipotoka,Tulipo na Tunapokwenda” 
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi.Sarah Mwaipopo ,akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa Mawakili wa Serikali yaliyokwenda sambamba na Maadhimisho ya miaka Mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali yaliyokuwa na kauli mbiu isemayo “Miaka mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Tulipotoka,Tulipo na Tunapokwenda” 
Mwakilishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu Zanzibar Bi.Fatuma Idd Ally,akitoa neno la Shukrani kwa niaba ya Ofisi ya Wakili Mkuu Zanzibar wakati wa ufungaji  mafunzo ya siku tatu kwa Mawakili wa Serikali yaliyokwenda sambamba na Maadhimisho ya miaka Mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali yaliyokuwa na kauli mbiu isemayo “Miaka mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Tulipotoka,Tulipo na Tunapokwenda” 
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi.Mary Makondo (hayupo pichani) wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa Mawakili wa Serikali yaliyokwenda sambamba na Maadhimisho ya miaka Mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali yaliyokuwa na kauli mbiu isemayo “Miaka mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Tulipotoka,Tulipo na Tunapokwenda” 
Na.Alex Sonna-DODOMA
Mawakili wa Serikali wametakiwa kutatua migogoro kwa njia ya majadiliano na Usuluhishi ili kutengeneza Mazingira mazuri yatakayowavutia wawekezaji kuja kuwekeza  nchini.
 
 
Hayo yamesema Jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi.Mary Makondo,wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa Mawakili wa Serikali yaliyokwenda sambamba na Maadhimisho ya miaka Mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali yaliyokuwa na kauli mbiu isemayo “Miaka mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Tulipotoka,Tulipo na Tunapokwenda” 
 
 
 Bi.Makondo amewataka mawakili wa serikali kuhakikisha wanatumia mafunzo hayo kwenda kuongeza ufanisi katika taasisi zao na kusaidia kupungunza migogoro na mrundikano wa kesi mahakamani kwa njia ya majadiliono.
 
 
“Nchi ikiwa na migogoro,kesi na matukio yasiyofaa hakuna maendeleo hivyo serikali inatambua kazi kubwa mnayoifanya ila kaongezeni kasi ya utatuzi wa migogoro ili kuwavutia Wawekezaji,”
 
 
Na kuongeza kuwa “Wawekezaji wanataka sehemu ambako hakuna ubabaishaji kwanza wanaangalia usalama wa uwekezaji wao sasa basi kawadhihirishieni wawekezaji kuwa Tanzania ni eneo salama la kuwekeza kwa kuendesha majadiliano na kutengeneza Mazingira mazuri ya uwekezaji fanyeni hili kwa maslahi mapana ya nchi na watanzania kwa ujumla,”amesema Bi.Makondo
 
 
Aidha Bi.Makondo  amesema kuwa dunia kwa sasa imehamia kwenye dijitali hivyo ni lazima Mawakili nao wageukie huko kwa kutumia teknolijia na akili bandia kutatua migogoro na kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani.
 
 
“Kwa sasa dunia imegeukia kwenye teknolojia sasa dijitali ndio inaongoza dunia hivyo hatuna budi na sisi kuelekea huku tutumie kurahisisha kazi na kutatua migogoro kwa wakati,”amesema Bi.Makondo
 
 
Pia ,amezishukuru taasisi zote zilizowaruhusu Mwawakili wa Serikali kuja kushiriki Mafunzo hayo ambayo imelenga kuwanoa ili waweze kuongeza ufanisi katika majukumu yao ya kila siku. 
 
 
Kwa upande wake Wakili Mkuu wa Serikali Dkt.Boniphace Luhende ameishukuru Wizara ya katiba na Sheria Kwa kushirikiana Bega Kwa Bega na Ofisi ya Wakali Mkuu wa Serikali na wadau wengine kuhakikisha Mafunzo hayo yanafanyika.
 
 
Dkt.Luhende amesema anaamini baada ya mawakili hao kunolewa kwa siku hizo tatu katika maeneo tofauti tofauti ikiwemo utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi na Majadiliano itakwenda kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani kwani utatuzi utafanyika kwa haraka kwa kuzingatia haki kwa pande zote mbili.
 
 
“Baada ya kunolewa kwa siku tatu naamini mmepata mambo mengi mapya sasa mkayatumia vyema kwa ajili ya ustawi wa taifa letu sitegemei tena kuona mrundikano wa kesi zisizoisha,katengenezeni Mazingira mazuri yatakayowavutia wawekezaji na mkasaidie eneo la manunuzi,”amesema Dkt.Luhende
 
 
Naye Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Sarah Mwaipopo Washiriki walikuwa 600 tangu Jumatatu na wameweza kupitishwa katika maeneo mbalimbali ambayo naamini yatawasaidia katika kazi zao.
Awali Mwakilishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu Zanzibar Bi.Fatuma Idd Ally,ameishukuru Ofisi ya Wakili Mkuu kwa kuendelea kushirikiana na Ofisi ya Zanzibar kwa kila hatua lengo ni kuleta ufanisi katika utendaji kazi.
”Mgeni rasmi tukuhakikishie mafunzo haya tuliyoyapata yataenda kuleta tija katika ufanisi wa kazi zetu huku Zanzibara kwa kuendelea kutatua utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi na Majadiliano itakwenda kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani”.amesema Bi.Fatuma

About the author

mzalendoeditor