Featured Kimataifa

RAIS SAMIA NA RAIS MUSEVENI WAZINDUA MRADI WA KUFUA UMEME MBARARA UGANDA

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya  Uganda Yoweri Museveni wamezindua Mradi wa Kufua Umeme wa Kikagati – Murongo, Mbarara nchini Uganda.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika Mradi wa Umeme wa Kikagati – Murongo, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kamba pamoja na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Kikagati – Murongo, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023. Mradi huo wa umeme utanufaisha nchi zote mbili katika masuala ya Nishati ya umeme.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakati alipotembelea mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo (Megawatt 16), Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.

Eneo la mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo pamoja na Mitambo kama linavyoonekana pichani, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakati wakisikiliza maelezo ya mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.

About the author

mzalendoeditor