Featured Kitaifa

NEC YAFANYA UTEUZI WA MADIWANI WATATU WANAWAKE WA VITI MAALUM

Written by mzalendoeditor
TUME ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC), imefanya uteuzi wa Madiwani watatu (3) Wanawake wa viti maalum kuziba nafasi zilizoachwa wazi katika Halmashauri tatu za Tanzania bara.
 
Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa kifungu cha 86A
(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 kikisomwa pamoja
na kifungu cha 35 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya
287 na kifungu cha 19 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura ya
288.
 
Taarifa ya Tume iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhan Kailima, imesema Tume imefanya uteuzi huo katika
kikao chake kilichofanyika tarehe 8 Mei, 2023 jijini Dodoma na kuteua Madiwani Wanawake Viti
Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
 
 imewataja madiwani walioteuliwa
kuwa ni Sina Jamaldin Nyanga wa Manispaa ya Lindi, Mary Muhjimy Kombe wa Wilaya
ya Morogoro na Mashavu Juma Barakabitse
wa Kigoma Ujiji.
 
Kailima amesema uteuzio huo
umefanyika  baada ya Tume kupokea taarifa
kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za mitaa kwa mujibu wa kifungu cha
13 (1) cha sharia ya uchaguzi ya serikali za mitaa sura 292, akiitaarifu tume
kuhusu uwepo wa nafasi wazi za madiwani wanawake wa viti maalum katika
Halmashauri tatu za Tanzania bara.
 
Nafasi hizo zimetokana na
vifo vya madiwani wanawake wa viti Maalum wa Kata husika. 

About the author

mzalendoeditor